MSIMISEKI SENIOR
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 459
- 287
Mimi ni mfugaji wa kuku, nguruwe na ng'ombe
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na utitiri wa maduka ya kutengeneza vyakula vya Mifugo ambayo havina ubora. Bahati mbaya watengenezaji hao hawana utaalam wowote juu ya mahitaji halisi ya wanyama hasa kuku.
Mara kadhaa nimenunua vyakula vinavyotengenezwa na watu waliopo mitaani kusema kweli havileti matokeo chanya mfano utagaji wa kuku au ukuaji wa kuku wa mayai ni mbaya na ukuaji wa kuku wa nyama ni mdogo sana
Binafsi imefika wakati ikabidi nitafute mtaalam wa Mifugo nimlipe anitengenezee fomula ambazo nikizitumia angalau ninapata matokeo kwa kiasi changamoto niliyonayo ni upatikanaji wa baadhi ya malighafi
OMBI
Naomba Serikali iweke usimamizi wa karibu kwa watu wanaoanzisha biashara ya kuchanganya chakula cha Mifugo kwani anayeumia ni Mfugaji kwa kupata tija ndogo
Ikiwezekana itoe elimu ya utengenezaji wa vyakula vya Mifugo na kuwapa vyeti wale wote wanaojihusisha na kuchanganya vyakula vya Mifugo au basi iwe inafanya ukaguzi ili kudhibiti ubora maana kuna wakati mtu unaenda kutengeneza chakula halafu unakutana na Dagaa zimeoza, Pumba hazieleweki, nk
Mnaohusika tafadhali fikisheni salaam hizi kwa WAZIRI WA MIFUGO