Formula gani nzuri kwa ajili ya kuku wa nyama?

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
Wakuu naombeni muongozo katika hili, nahitaji kujua jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku wa nyama (broiler).

Vyakula vya kuku wa nyama Vimepanda maradufu halafu soko la Kuku hilo pia linasumbua.

Tafadhali mwenye kujua formula ya utengenezaji wa chakula hicho na kuku akakua vizuri. Na kama kuna aliuewahi kutumia njia hiyo. Naombeni uzoefu wenu.

Asanteni.
 
Asante, ikifika ile hatua ya mwisho ntawapa nini, Yan finisher?
Mie Nina ujuzi na chotara na kuku wa Malawi. Nawafuga hao sijawahi jaribu broiler

Ila sasa mchanganyiko wa broiler uko tofauti. Nenda ubungo pale waarabu wanauz vyakula quality sana. .

Wakati naandika nimeamuwa kuwapigia simu dada mmoja muuzaji wa vyakula vya kuku. Anasema dawa zake zinauzwa Bei sana zankuchanganyia kwenye chakula. Anasema broiler chakula kinauzwa 81000, na finisher inauzwa 82000. .

Wadau wavivu kuchangia Uzi kama hizi mda wote naona hawataki kutoa maarifa. .

Ila kashauri Bora ununue chakula dawa za kuchanganya ni Bei sana. Sasa sijajua anamaanisha kuwa perhaps it will not be cost effective. .

Hicho chakula nilichokutajia ni kwa ajili ya kuku wa kawaida sio broiler. Kama una mpango wa kuwala tu nyumbani ila kibiashara tuwasubiri wataalam waje. .
 
Nimepiga simu Farmers center niongee na daktari wa mifugo. Naweza kukupa number zao kama reference. .
Nimejibiwa kile chakula Huwa wananunua special. Kasema usichanganye mwenyewe kina formula kubwa sana ukikosea kuku wanadumaa hawakui. Hivyo Dr kashauri uende ununue kilichochanganywa la sivyo utapata hasara kubwa. .
 
Asante sana kwa ushauri huo
 
Kuku wa nyama (broiler) wanatesa sana
Ila pia wana faida kubwa sana. Hata Mimi nilitaka kufuga ila kilichonishinda ni gharama za kuwatunza hizo week nne. Usiku kuamka kuwaangalia au kuhakikisha wana joto sahihi. Nikaona Bora nifuge kuroiler na Malawi. .

Ina maana huko uliko Hakuna wanaouza vyakula vya broilers?
 
Wapo sana tu sema ni vile kutaka kusave, vyakula vyake bei sana, isitoshe pia kuna kutetereka kiuchumi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom