Kwa heshima na taadhima, sio mbaya nikiwaaga members wenzangu ambao nimefahamiana nao hapa JF. Pia, kwa dhati kabisa naomba wote wenye niliwakwaza kwa makusudi ama kwa bahati mbaya wanisamehe.
Siamini kama kuna yeyote anaeye tamani kuhitimisha safari yake hapa duniani akiwa mwenye dhambi, kwasababu Mungu wetu mwenye upendo ametupa nafasi ya kutubu dhambi zetu siku zote.
Baada ya kazi sasa nimeona nijitenge kwa muda wa siku kadhaa ili niitazame afya yangu. Kama Mungu akipenda basi tutaendelea kujiona tena, lakini akinipenda zaidi basi yote kheri.
Hakika ninaogopa, nimekuwa na hofu kuu, moyo wangu unahuzunika.
Ngoja nipambanie hii pumzi.
Sent using
Jamii Forums mobile app