Naomba nisaidiwe jamani kisheria

shegaboy

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
213
34
Mimi ni muajiriwa katika kampuni fulani hapa mjini. nilipewa mkataba wa miaka minne, ambayo mpaka sasa nimeshatumikia mwaka mmoja na nusu. wanasema kuwa kutokana na matatizo ya fedha wanataka kupunguza watu. je katika kupunguza wanalipa ila kwa sasa hawana fedha hivyo muende mpaka watakapo pata fedha ndio watalipa:
1. mafao
2. likizo zako
3. mishahara unayodai na nyongeza zako za mishahara

Je vipi kuhusu mkataba wangu awalipi chochote kwani mkataba wangu ulikuwa wa kipindi maalumu yaani wenye ukomo hapa sija lielewa.

pia taratibu za kupunguza watu zikoje maana walikuja wao na mwanasheria wao tu. wakatoa baadhi ya sheria na sisi hatujajiunga katika chama chochote cha wafanya kazi.
 
kaka pole sana kwa matatizo,inatakiwa mjiunge nyote mnaopunguzwa kazi mtafute mwana sheria awasaidie kwani kuna kitu kinaitwa Low of contract ni sheri ya mikataba ,huyo mwajiri kavunja makubaliano yenu mna haki ya kudai na mkalipwa haki stahiki msiogope haki haiji mara moja itawachukua muda ili mtapata.
 
pole sana ndugu,
1. kati ya hao waliopunguzwa na wewe umo?

2. kama umo, ni kwamba watatakiwa wakulipe kwa kuvunja mkataba na wala haina kukwepa kwa sababu ni matatizo yao wao na sio yako, na pia sheria inaruhusu kuvunja mkataba kama shughuli ulizao kuwa unafanya ziimeisha au zimesitishwa au haziendelei tena

3. swala la jinsi ya kupunguza sio ishu sana, cha msingi ni wewe kulipwa kwa mkataba kuvunjwa kwa kuwa project haiendelei tena. au wakulipe stahili zako zote kwa hesabu ya miaka yote minne ya ajira yako kama wataweza.
 
Emock
Nashukuru kwa kuniondoa wasiwasi ni kweli na mimi naweza kuwepo kwani wanaotakiwa kutolewa huko ni wengi sio wawili au watatu ila kama kumi na hivi. Unajua mwajiri wetu ni mtu mgumu sana anacho taka yeye sisi tuondoke ila kampuni yake ibaki hicho ndio shida. anataka kuwaondoa watu wasio waanzilishi wa hiyo kampuni. Ila tunamshukuru sana Mungu yeye ndiye mlinzi na mpiganaji juu yetu, nalitambua kutafuta haki yako kunaitaji kujitoa na kupigana kweli kweli sio kuzubaa. Na najua unapodai haki yako au kutaka kujua haki yako kuna mengi yatajitokeza ila niko tayari kukabiliana nayo.
 
CONGOBE
Nashukuru sana NIKWELI HAKI INATAFUTWA HUWEZI KUKAA NA KUIONA INAKUAJA KWAKO ILA KWA KUPIGANA NASHUKURU SANA. NDICHO TUNACHOSUBIRI KAMA TUTAPATA HIZO BARUA TUTAJIUNGA KWA WALE WATAKAO PENDA UNAJUA TUKO TOFAUTI WENGINE NI WATU WA KUPOTEZEA ILA HAKIA YA MTU AOPOTEI INGAWA ITACHELEWA.
 
Kama wamevunja mkataba wako wa ajira kienyeji wanatakiwa wakulipe, nenda sehemu za sheria upate msaada.
 
Ukisoma Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, 2004 kwa pamoja na Kanuni za Utendaji Bora, 2007 utaona kuwa utamaduni wa zamani wa waajiri kuajiri na kufukuza, yaani, hire and fire unakatazwa na sheria na hivyo mwajiri, si tu anatakiwa kuwa na sababu za msingi za kumuachisha mwajiriwa kazi lakini pia sababu hizo ni lazima ziwe halali kisheria na ni lazima afuate utaratibu halali.

Katika mazingira uliyoyataja mwajiri anaweza kukuachisha kazi kutokana na mahitaji ya kiuendeshaji lakini kabla ya kufanya hivyo ni lazima afanye mashauriano na wafanyakazi ambao wanaweza kuathiriwa na zoezi hilo. Kama hajafanya mashauriano basi atakuwa amekiuka utaratibu halali.

Mwajiri anapoamua kumuachisha mwajiriwa kazi ni lazima amlipe malipo yafuatayo:-
  • Mshahara wa kazi aliyoifanya kabla ya kuachishwa;
  • Malipo ya likizo ya mwaka ambayo mwajiriwa hajachukua;
  • Malipo ya likizo ya mwaka kwa mzunguko wa likizo ambao bado haujakamilika;
  • Malipo ya notisi (mshahara wa mwezi mmoja);
  • Malipo ya kazi iliyofanywa wakati wa muda wa ziada, sikukukuu na muda wa usiku (ambayo hayajalipwa).
  • Kiinua mgongo; na
  • Malipo ya usafiri hadi mahali alipochukuliwa wakati wa ajira.
 
kaka usijali sana chukulia kama mchezo flani ila hakika mtafanikiwa a mimi nina matatizo ila najua nitashinda kwani wamejaribu hata kuniweka lock up niach madai yangu wamechemka kheri kufa ukipigana kuliko kufa ukiomba msamaha
 
Ukisoma Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, 2004 kwa pamoja na Kanuni za Utendaji Bora, 2007 utaona kuwa utamaduni wa zamani wa waajiri kuajiri na kufukuza, yaani, hire and fire unakatazwa na sheria na hivyo mwajiri, si tu anatakiwa kuwa na sababu za msingi za kumuachisha mwajiriwa kazi lakini pia sababu hizo ni lazima ziwe halali kisheria na ni lazima afuate utaratibu halali.

Katika mazingira uliyoyataja mwajiri anaweza kukuachisha kazi kutokana na mahitaji ya kiuendeshaji lakini kabla ya kufanya hivyo ni lazima afanye mashauriano na wafanyakazi ambao wanaweza kuathiriwa na zoezi hilo. Kama hajafanya mashauriano basi atakuwa amekiuka utaratibu halali.

Mwajiri anapoamua kumuachisha mwajiriwa kazi ni lazima amlipe malipo yafuatayo:-
  • Mshahara wa kazi aliyoifanya kabla ya kuachishwa;
  • Malipo ya likizo ya mwaka ambayo mwajiriwa hajachukua;
  • Malipo ya likizo ya mwaka kwa mzunguko wa likizo ambao bado haujakamilika;
  • Malipo ya notisi (mshahara wa mwezi mmoja);
  • Malipo ya kazi iliyofanywa wakati wa muda wa ziada, sikukukuu na muda wa usiku (ambayo hayajalipwa).
  • Kiinua mgongo; na
  • Malipo ya usafiri hadi mahali alipochukuliwa wakati wa ajira.

Nashukuru kwa ushauri wako kaka Bandio. unapewa barua ya kuitwa kwenye kikao cha kujadili ili kuepuka kupunguza kazi na kisha hapo hapo mnafikia hatua ya kuambiwa kuwa tunakwenda kupunguza watu basi. na unapewa tarehe kuwa tarehe fulani tutataja majina ya watakao punguzwa na kupewa barua zao. kisha mnakwenda mtakuja kulipwa baada ya sisi kupata fedha kwa kuwa sasa atuna pesa na mkataba weneyewe ndio kwanza umetumikia mwaka mmoja na nusu. kweli inaingia akilini na niyeye aliyekupa huo mkataba na kukwambia kuwa nimekupa mkataba mrefu ili uendee ukakope bank, na yeye leo ndio mdhamini wa mkopo wangu bank. imekaaje hapo Bandio
 
Hapa cha kufanya...jikusanyeni wote mliopunguzwa ajira..nendeni kwa mwanasheria..atafungua madai yenu kwa pamoja..CMA..mtaanza na mediation, then abitration..ikishindikana huko CMA then mnakwenda mahakama kuu..lakini ni kinyume cha sheria kwa muajiri kuwanyima haki ya kujiunga na vyama vya wafanyakazi...hii ni mojawapo ya haki za msingi kabisa kwa mfanya kazi yoyote yule katika idara yoyote..alijua nini kitafuata ndio maana akawanyima kufanya hivyo...inaonekana ni msanii kweli..mkipeleka madai yenu huko CMA , then Baraza ndio litakalo amua kuwa mnahaki ya kulipwa stahili zenu, zipi, na kwa wakati gani sio kwa mwajiri kuwapangia lini atafanya malipo..kuna hitajika kuwe na time frame ya kufanya hayo malipo na si kusema tu nendeni halafu tutawaita kuwalipa..ikiwa milele je?? hapa ndipo kwenye tatizo..na mahali pa kutatuz hili tatizo ni mahakamani...haraka!!!!
 
Nashukuru kwa ushauri wako kaka Bandio. unapewa barua ya kuitwa kwenye kikao cha kujadili ili kuepuka kupunguza kazi na kisha hapo hapo mnafikia hatua ya kuambiwa kuwa tunakwenda kupunguza watu basi. na unapewa tarehe kuwa tarehe fulani tutataja majina ya watakao punguzwa na kupewa barua zao. kisha mnakwenda mtakuja kulipwa baada ya sisi kupata fedha kwa kuwa sasa atuna pesa na mkataba weneyewe ndio kwanza umetumikia mwaka mmoja na nusu. kweli inaingia akilini na niyeye aliyekupa huo mkataba na kukwambia kuwa nimekupa mkataba mrefu ili uendee ukakope bank, na yeye leo ndio mdhamini wa mkopo wangu bank. imekaaje hapo Bandio

Nadhani mwajiri wenu hayuko tofauti na waajiri walio wengi, ambao hupenda kutumia udhaifu wa wafanyakazi walio wengi wa kutojua haki zao kuwakandamiza. Ni vizuri wafanyakazi wakajitahidi kujua sheria za kazi ili waweze kuzitetea inapolazimu. Na nafikiri wakati umefika waandaaji wa mitaala ya vyuo wafikirie uwezekano wa sheria za kazi kufundishwa kwa wanafunzi wote wa vyuo.

Kwa maelezo yako inaonyesha kuna ukiukwaji wa taratibu katika zoezi la kuwapunguza kazi, nashauri muungane wote ambao mmeathiriwa na hilo zoezi kisha mtafute wakili atawashauri nini cha kufanya.

Suala la kutumikia mkataba mwaka mmoja na nusu ni irrelevant kwani sheria inampa mwajiri uwezo wa kumwachisha mwajiriwa kazi, ilimradi awe na sababu halali na za msingi, afuate utaratibu halali na amlipe stahili zake.
 
Back
Top Bottom