Naomba nikuroge mume wangu

Naomba nikuroge mume wangu

Inawezekana na wewe kashakuroga..mwanamke mchawi no kwa kweli ni wa kuacha
 
Blaza na wewe jiandae kwa hilo very soon......
 
Wanawake wengi wanaamini katika kuwashika wanaume. Hii ndio sababu mkeo haoni tatizo hapo.
 
Wanawake wengine Sijui mnawatoaga wapi! Au mnakua mnausingizi????
 
teh teh huenda wewe umerogwa sana tu sema ni kisiki cha mpingo
 
Hayo mambo ya kurogana, mwisho wa siku ndugu yako atakua chizi kama anakinga dhabiti ya Mwenyezi Mungu.
 
Habari zenu wakuu,

Leo nimepokea simu ya mdogo wangu akinipa taarifa ya kuachana rasmi na aliyekuwa mkewe madai kuwa mkewe alikuwa akimfanyia vitendo vya ushirikina (limbwata) na mambo yanayo husiana na urozi kiasi cha mdogo wangu kukabidhi mshahara wote kwa mkewe kila apatapo, kumuogopa amuonapo na kushindwa kujiamini.

Mimi binafsi sikuweza kumshauri aachane nae ila nikamwambia awaeleze wazazi maana huenda wao wakawa na jibu zuri au ushauri sahihi zaidi kilichonifanya niandike uzi huu ni kuwa, baada ya kulifikiria sana suala hili nikaona bora nimshirikishe mke wangu kwa kumueleza kisa kizima cha shemeji yake na mkewe.

Jibu alilonipa mke wangu limenishangaza jamani nanukuu ''HAKUNA TATIZO HAPO MUME WANGU, KAMA MKEWE KAMROGA ILI AMPENDE MBONA NI VIZURI KWANI HUENDA MDOGO WAKO ALIKUWA NA MICHEPUKO. MWAMBIE AMRUDISHE TU WALA ASIMUACHE KWANI ALIKUWA AKIMSAIDIA ILI AMPENDE YEYE TU'' Mwisho wa kunukuu.

Jamani mimi nimebaki nimeduwaa maana sijui niseme nini kwa huyu mke wangu, yeye anaona yuko sawa na wala hana wasiwasi na kauli hiyo.Kama ndo ungekuwa wewe ndugu yangu ungefanyeje?
Hata wewe usharogwa tayari
 
Mnaoshabikia huyo mke kumpa limbwata mumewe hamjui hilo limbwata ni kitu gani, ni uchafu uliovuka mipaka..

Huyo amelishwa nyama chafu na shahawa za mbwa hadi zikamkolea..
 
Back
Top Bottom