Naomba nikuroge mume wangu

Naomba nikuroge mume wangu

jangala

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
1,583
Reaction score
2,383
Habari zenu wakuu,

Leo nimepokea simu ya mdogo wangu akinipa taarifa ya kuachana rasmi na aliyekuwa mkewe madai kuwa mkewe alikuwa akimfanyia vitendo vya ushirikina (limbwata) na mambo yanayo husiana na urozi kiasi cha mdogo wangu kukabidhi mshahara wote kwa mkewe kila apatapo, kumuogopa amuonapo na kushindwa kujiamini.

Mimi binafsi sikuweza kumshauri aachane nae ila nikamwambia awaeleze wazazi maana huenda wao wakawa na jibu zuri au ushauri sahihi zaidi kilichonifanya niandike uzi huu ni kuwa, baada ya kulifikiria sana suala hili nikaona bora nimshirikishe mke wangu kwa kumueleza kisa kizima cha shemeji yake na mkewe.

Jibu alilonipa mke wangu limenishangaza jamani nanukuu ''HAKUNA TATIZO HAPO MUME WANGU, KAMA MKEWE KAMROGA ILI AMPENDE MBONA NI VIZURI KWANI HUENDA MDOGO WAKO ALIKUWA NA MICHEPUKO. MWAMBIE AMRUDISHE TU WALA ASIMUACHE KWANI ALIKUWA AKIMSAIDIA ILI AMPENDE YEYE TU'' Mwisho wa kunukuu.

Jamani mimi nimebaki nimeduwaa maana sijui niseme nini kwa huyu mke wangu, yeye anaona yuko sawa na wala hana wasiwasi na kauli hiyo.Kama ndo ungekuwa wewe ndugu yangu ungefanyeje?
 
Teh, kama wamezoeana ujue anajua na pengine walishauriana, sio kwa kumtetea huko jamani
 
Yule shemeji yako yupo sahihi tu kumloga baba watoto wake muache labda dawa haijashika vizuri atamrudsha tu
 
Hata wewe mkuu umesharogwa...hiyo sio akili yako kuleta mambo ya mdogo wako kwa wife...kimbilia kanisani uokoke na utafunguliwa..
 
Ok pole mkuu swala zima la kufanyiwa libwata na me halikubaliki. Kumbuka mliingia katika ndoa kwa kupendana nyinyi wenyewe. Hapa kinachohitajika ni kuaminiana na kulinda ndoa yenu. Baba uwe mwaminifu kwa kutimiza majukumu ya kifamilia utaona mwanamke mwenyewe anakuamini na yeye kufanya yaliyo ya upande wake na maisha utaona yanakwenda kwa furaha hapo nyumbani hata mambo ya mwanamke kuwaza kimbwata hayatakuwepo
 
Back
Top Bottom