Shadow7
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 13,757
- 20,141
Great thinkers naomba ufafanuzi juu ya haya maswali machache kuhusu biblia takatifu.
1. Hesabu 23:19 "inasema Mungu si mtu, aseme uongo, wala si mwanadamu ajute Iwapo amesema hatalitenda? Iwapo amenena hatalifikiliza?"
1 Samweli 15:10 "Ndipo neno la BWANA likamjia Samweli, kusema,
[11]Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha."
Swali langu lipo hapo nilipopawekea rangi. Je, Mungu anajuta?
2. 1 Samweli 16:14 "Basi, Roho ya BWANA ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa BWANA ikamsumbua."
Swali ni je, BWANA ana roho mbaya?
3. Marko 9:1 BHN. Yesu akaendelea kuwaambia, “Kweli nawaambieni, wako wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa enzi.”
Swali Je baadhi ya watu waliokuwepo kippindi cha Yesu hawatakufa mpaka kurudi kwake?
4. MATENDO YA MITUME
Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,
2 akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
3 Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni.
4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi?
5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.
6 Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.
7 Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu.
8 Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.
9 Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.
6 Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.
7 Nikaanguka nchi, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi?
8 Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi.
9 Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami.
10 Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uingie Dameski, na huko utaambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa uyafanye.
Swali : Kwanini paulo aseme uongo?
5. UFUNUO WA YOHANA
Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
Je, watakaoingia mbinguni ni 144000 tu? rejea pia LUKA
Naomba kueleweshwa.
1. Hesabu 23:19 "inasema Mungu si mtu, aseme uongo, wala si mwanadamu ajute Iwapo amesema hatalitenda? Iwapo amenena hatalifikiliza?"
1 Samweli 15:10 "Ndipo neno la BWANA likamjia Samweli, kusema,
[11]Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha."
Swali langu lipo hapo nilipopawekea rangi. Je, Mungu anajuta?
2. 1 Samweli 16:14 "Basi, Roho ya BWANA ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa BWANA ikamsumbua."
Swali ni je, BWANA ana roho mbaya?
3. Marko 9:1 BHN. Yesu akaendelea kuwaambia, “Kweli nawaambieni, wako wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa enzi.”
Swali Je baadhi ya watu waliokuwepo kippindi cha Yesu hawatakufa mpaka kurudi kwake?
4. MATENDO YA MITUME
MLANGO 9
Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,
2 akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
3 Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni.
4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi?
5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.
6 Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.
7 Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu.
8 Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.
9 Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.
MATENDO YA MITUME
MLANGO 22
5 Kama Kuhani Mkuu naye anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipokea barua kwao kuwapelekea ndugu wale, nikaenda Dameski, ili niwalete wale waliokuwa huko hata Yerusalemu, hali wamefungwa, ili waadhibiwe.6 Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.
7 Nikaanguka nchi, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi?
8 Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi.
9 Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami.
10 Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uingie Dameski, na huko utaambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa uyafanye.
Swali : Kwanini paulo aseme uongo?
5. UFUNUO WA YOHANA
MLANGO 14
Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
Je, watakaoingia mbinguni ni 144000 tu? rejea pia LUKA
MLANGO 12:32 Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.
Naomba kueleweshwa.