Naomba mwenye uzoefu na vifaa vya saluni ya kiume

Ruyama

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
367
561
Nina wazo la kufungua saluni ya kiume, lakini sijui mashine ya kunyoa ni bei gani,kiti na kioo, kuhusu redio nitanunua sabufa, naombeni mawazo ndugu zangu na bado kijana atakaye kuwa kinyozi huwa analipwaje? sharing is caring sitaki kukurupuka.
 
Kijana uwa anajilipa mwenyewe ila we mnakubaliana hela flan akupe kwa wiki
 
Nina wazo la kufungua saluni ya kiume, lakini sijui mashine ya kunyoa ni bei gani,kiti na kioo, kuhusu redio nitanunua sabufa, naombeni mawazo ndugu zangu na bado kijana atakaye kuwa kinyozi huwa analipwaje? sharing is caring sitaki kukurupuka.

Unataka saloon ya aina gani? ya kisela tu au barbershop kabisa?
 
Salon ya kisela tuu

Sawa! Apo utahitaji viti viwili Tzs 320,000
Utahitaji kodi ya frame (gharama inategemea na upo wapi)
Frame kama haina mlango wa vioo na unauhitaji andaa Tzs 550,000 pamoja na stickers zake Tzs 35,000.

Utahitaji vioo viwili(at least kwa kuanzia cha mbele na nyuma) Tzs 200,000

Kitu cha kukalia wateja Tzs 150,000

Kabati Tzs 100,000

Machine nzuri na imara ni Homecut na Wahl Tzs 130,000 moja.. zipo za Tzs 80,000(wahl) pia sio mbaya! utahitaji mbili

Vikolokolo vingine kama mataulo,powder,spirit etc unaeza andaa Tzs 45,000

Pia ongeza na gharama za radio au Tv au vyote!

Jumla ni kama Tzs 1,400,000 ukiongeza na kodi inaweza fika Tzs 1,700,000.
 
Pia ongeza na gharama za radio au Tv au vyote

Jumla ni kama Tzs 1,400,000 ukiongeza na kodi inaweza fika Tzs 1,700,000.

Pia kuna gharama zitakazoongezeka kama rangi na vitu vingine vya hapa na pale! pia nilisahau gharama ya feni(kwa dar es salaam ni muhimu sana)
 
Sawa! Apo utahitaji viti viwili Tzs 320,000
Utahitaji kodi ya frame (gharama inategemea na upo wapi)
Frame kama haina mlango wa vioo na unauhitaji andaa Tzs 550,000 pamoja na stickers zake Tzs 35,000.

Utahitaji vioo viwili(at least kwa kuanzia cha mbele na nyuma) Tzs 200,000

Kitu cha kukalia wateja Tzs 150,000

Kabati Tzs 100,000

Machine nzuri na imara ni Homecut na Wahl Tzs 130,000 moja.. zipo za Tzs 80,000(wahl) pia sio mbaya! utahitaji mbili

Vikolokolo vingine kama mataulo,powder,spirit etc unaeza andaa Tzs 45,000

Pia ongeza na gharama za radio au Tv au vyote!

Jumla ni kama Tzs 1,400,000 ukiongeza na kodi inaweza fika Tzs 1,700,000.
Wabeja sana ngosha
 
Nina wazo la kufungua saluni ya kiume, lakini sijui mashine ya kunyoa ni bei gani,kiti na kioo, kuhusu redio nitanunua sabufa, naombeni mawazo ndugu zangu na bado kijana atakaye kuwa kinyozi huwa analipwaje? sharing is caring sitaki kukurupuka.

Malipo kwa kijana unaweza kubaliana kwa namna mbili, awe anakupa hela kwa siku au week (mfano 35K kila week).

Mnaweza pia kubaliana wewe ndio uwe unampa mshahara kwa mwezi (labda 200k), hii ni ngumu maana utahitaji kuwepo au kuwa na msimamizi golini.

Pia ili kummotivate kijana unaweza mpa ata week moja ya free road, asikulipe kitu ila na wewe uwepo kufatilia biashara inavokwenda kabla hujampangia gharama ya yeye kukulipa.
 
Njema sana hii
 
Sawa! Apo utahitaji viti viwili Tzs 320,000
Utahitaji kodi ya frame (gharama inategemea na upo wapi)
Frame kama haina mlango wa vioo na unauhitaji andaa Tzs 550,000 pamoja na stickers zake Tzs 35,000.

Utahitaji vioo viwili(at least kwa kuanzia cha mbele na nyuma) Tzs 200,000

Kitu cha kukalia wateja Tzs 150,000

Kabati Tzs 100,000

Machine nzuri na imara ni Homecut na Wahl Tzs 130,000 moja.. zipo za Tzs 80,000(wahl) pia sio mbaya! utahitaji mbili

Vikolokolo vingine kama mataulo,powder,spirit etc unaeza andaa Tzs 45,000

Pia ongeza na gharama za radio au Tv au vyote!

Jumla ni kama Tzs 1,400,000 ukiongeza na kodi inaweza fika Tzs 1,700,000.
Asante sana! Kama ni Barbershop inakuwaje?
 
Malipo kwa Barbershop wanavyofanya baadhi ya saloon kwa siku hizi. Kama mteja kaja na gharama ya kunyoa ni 3000 basi 1000 anachukua kinyozi 2000 inaenda kwa mwenye saloon.
 
Naombeni kujua kwa wenye uzoefu wa biashara hii ya saloon ya kiume kuanzia mtaji wa kawaida na mpaka vifaa na maingizo ya pesa.
 
Back
Top Bottom