Naomba muongozo wa usafiri wa treni Mbeya - Dar es Salaam

Nilisafiri mwaka 2001 kwa treni ya Tazara, nilienda kwa free pass , KUSAFIRI na Treni ni raha sana, aswaa ukate ticket ya first class, tulikula bia na wadada wa kizambia, tuli-Enjoy ile safari kwakweli
Aisee hongera mkuu ndo kitu nataka nijifunze pia nione utofauti japo najua nitachelewa kufika tofauti na basi!
 
Kwa maelezo haya nishaiona sfr yangu vile itakuwa nashukuru Sana mkuu umefafanua vzr Sana Sana
ubarikiwe na Imani na wengine wasojua wamepata kitu pia!
 
Asante bujibuji
 
Kna cku natka dar naenda moro ,nakumbuka nilikula tungi(pombe) njia nzima mpka kufika ifakara hoi hoi al manusura nipitilize kituo...ila nilichana mdomo cku iyo baada ya kuanguka kisa tungi, mbna nilikoma
Pole sana mkuu ata hvyo ulijitahidi mana mi nawaza kutokula chochote nisije rudisha chenji
SFR ya Kwanza Kwa huu usfr inabidi niwe mtulivu
 
Ukikosa 1st class huko third jiandae kupanda na mbuzi,majogoo,mikungu ya ndizi na usishangae kuona watu wanasimama ifakara to mbeya mana kunajaa kama umepanda mwendo kasi😂😂
 
Kwa mkoa mpenzi...

Ila kama unajua train fare kwa chumba kizima cha first class naomba kujua.
Oohh kwa Mbeya hotels nzuri jaribu Desderia, Tughimbe, Hills View, Peace of Mind, Mbeya Hotel na Usungiro

Nauli Dar-Mbeya kwa Express train first class per bed ni 47K na chumba kimoja kina vitanda vinne so ukitaka chumba kizima utalipa 47K mara nne. Kwa Ordinary train first class ni around 39K nako ni vitanda vinne so utalipa 39K mara nne.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…