Naomba muongozo wa usafiri wa treni Mbeya - Dar es Salaam

Usafiri wa train ni usafiri ninaoupenda sana...ni usafiri wenye risk ndogo na wa uwakika ukilinganisha na bus.

Kuhusu train via TAZARA zipo za aina mbili.
1. Train ya mizigo
2. Train ya abiria

~ Train ya abiria zipo za aina mbili

1* Express train...hii ni train ya route ndefu safari yake huanzia Zambia to Dar,sifa ya train hii Ina speed,inasimama vituo muhimu tu,inamuinekano mzuri kwa ndani,inabeba mizigo kwa limit, pia nauli yake imechangamka kidogo...

Ina madaraja matatu.
First....ni kachumba chenye vitanda vinne au viwili vya kukunja na kukunjua na meza moja..ni daraja lililo karibu na sehemu ya vinywaji na chakula, system charging na feni ipo na vyoo vyake vipo vzur sana.

Ni daraja lenye Bei ya juu kuliko class zote,ukipanda daraja hili hutojutia safari yako.

Second class..ni daraja la kati kuna seat ambazo zpo comfortable (super seat) na zpo seat zengne zinafanana tu na third class,kila behewa Lina system charging moja...kila behewa Lina feni 6,vyoo vyake vipo poa.
Bei yake ya kawaida tu,kama utapanda second class kata ticket ya super seat hutojutia safari yako.

Third class...halina tofauti sana na second class. Na Bei yake ndogo kulinganisha na first na second.

2* Ordinary train....hii train huanzia mbeya to Dar,ni train ambayo huchukua muda mrefu ktk safari zake,husimama kila ktuo ata porini as long as kuna huduma maalumu inahitaji kufanyika.

Nayo Ina class tatu, first.. second..na third.

Nauli yake hupishana elfu 2 adi elfu 5 na express.

Ukipanda ordinary sikushauri ata kidogo upande third class.
Kwa maelezo haya nishaiona sfr yangu vile itakuwa nashukuru Sana mkuu umefafanua vzr Sana Sana ubarikiwe na Imani na wengine wasojua wamepata kitu pia!
 
Asante bujibuji
 
Kna cku natka dar naenda moro ,nakumbuka nilikula tungi(pombe) njia nzima mpka kufika ifakara hoi hoi al manusura nipitilize kituo...ila nilichana mdomo cku iyo baada ya kuanguka kisa tungi, mbna nilikoma
Pole sana mkuu ata hvyo ulijitahidi mana mi nawaza kutokula chochote nisije rudisha chenji SFR ya Kwanza Kwa huu usfr inabidi niwe mtulivu
 
Ukikosa 1st class huko third jiandae kupanda na mbuzi,majogoo,mikungu ya ndizi na usishangae kuona watu wanasimama ifakara to mbeya mana kunajaa kama umepanda mwendo kasi😂😂
 
Kwa mkoa mpenzi...

Ila kama unajua train fare kwa chumba kizima cha first class naomba kujua.
Oohh kwa Mbeya hotels nzuri jaribu Desderia, Tughimbe, Hills View, Peace of Mind, Mbeya Hotel na Usungiro

Nauli Dar-Mbeya kwa Express train first class per bed ni 47K na chumba kimoja kina vitanda vinne so ukitaka chumba kizima utalipa 47K mara nne. Kwa Ordinary train first class ni around 39K nako ni vitanda vinne so utalipa 39K mara nne.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom