Naomba msaada wa tatizo hilI ukutani

upeo

JF-Expert Member
Jun 10, 2013
356
207
Habarini wakuu naomba msaada wa tatizo langu hilo kwenye ukutani.

Je, ni tiba gani inafaa hapo ili tatizo liondoke moja kwa moja?

Shukrani.

IMG-20230227-WA0009.jpg
IMG_20230227_082135.jpg
 
Wakati wa ujenzi uliweka yale lile nailoni la kuzuia maji maji yasipande ukutani?
Nyumba yako ilipo ilikuwa ni eneo la maji kutuhama?
Kuna mabomba yamepita ndani ya kuta eneo hilo?
Mkuu hii nyumba nimenunua ishapigwa msingi tayari

Mtihani upo hapo siwezi kujua kama iliwekwa dawa au vipi
 
Hiyo ratio iliotumika kupiga plasta ni mbovu sana...
Japo ni fungus lakini plasta na skimming ni mbovu sana....hii ni jenga uza..
Nunua white skim..fundi apige mikono mitatu, kama unataka na dawa ya fungus wanayo pia.

Angepiga plasta vizuri, hyo powder ingekuwa inabanduka bila cement
 
Nashukuru mkuu nitafanya hivyo
 
naam mkuu chumvi kwa kweli ipo
Kama ni issue ya chumvi, fumua plaster yote na ipingwe upya kwa mchanganyiko mkali sana, yaani unaweza fanya 1:2, Yaani kipimo kimoja cha cement kiende sawa na vipimo viwili vya mchanga. Pia mchanga usiwe na hao magadi.( unaweza chukua sample ukapeleka Tanroads wakakupimia bei yake ni ya kawaida kabisa).
Wakati wa rangi mwambie fundi wako atumie binder.
 
Back
Top Bottom