Kwa yeyote anayejua source au origin au yanakotokea (mkoa, wilaya hata ikiwezekana vijiji maarufu kwa kilimo cha) matikiti na mapasion yanayoletwa hapa Dar es salaam.
Mkuranga na Rufiji zinachangia sana haya mazao mawili kwa kiasi kikubwa sana, kwa mfano vijiji vyote vilivyo ktk njia ya Vikindu mpaka Tundwi Songani Mkuranga,Ukanda wa Malela mpaka Shungubweni,maeneo ya Pemba mnazi,kididimo,Kisele kote huko matunda haya yanamea vizuri.
Bonde la Ruvu linatoa sana tikiti, au bonde la Wami pia. Maeneo ya Mufindi Iringa kuna passion nyingi sana ila zimekosa soko kabisa.