Naomba msaada wa kutofautisha Engine 1G-FE na VVTi

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,553
3,070
Habari,

Naomba msaada kujua tofauti ya ENgine kati ya 1G-Fe ukilinganisha na VVti kama zote ni CC 2000.

Please naomba msaada maana nahitaji kufanya maamuzi ya haraka.

Ahsanteni sana
 
vvti ni very economical ila sijui uimara wake

Vvti ni engine nzuri tatizo bado mafundi walio wengi bado hawajajua kuzirekebisha pindi zinapopata hitilafu. Ndio maana wengi wnapendelea 1G FE ( 1G kavu ) kwa kuwa wengi wameshazijulia pindi zinaposumbua. Kwa uimara na utumiaji wa mafuta vvti ni nzuri zaidi
 
Hata spare za 1g fe utazipata kirahis kuliko za vvti engine hebu kajaribu kuulizia overhaul ya 1g na vvti ni ipi utaipata kwa haraka
 
Hata spare za 1g fe utazipata kirahis kuliko za vvti engine hebu kajaribu kuulizia overhaul ya 1g na vvti ni ipi utaipata kwa haraka

Tatizo letu watanzania ni watu wa kuropoka with no core evidence/arguments, ukimuuliza mtu kwa nini injini za Vvti au D4 ni kimeo anakua hana jibu la kukuambia, kiukweli vvti na D4 ndo current modified features za injini ambazo ziko effective na efficient kwa kila kitu yaani nguvu, mwendo, ulaji wa mafuta na uhimili wa kazi, mi mwenyewe nnayo toyota allex vvti moto wake usipime,
 
VVT i variable valve Timing with intelligence D4 ni injini bora na ya kisasa very economy.. Tatizo la mafundi wetu wengi ni wale waliokimbia shule wakajifunza mitaani.. hawataki kujifunza vitu vipya
 
Tatizo letu watanzania ni watu wa kuropoka with no core evidence/arguments, ukimuuliza mtu kwa nini injini za Vvti au D4 ni kimeo anakua hana jibu la kukuambia, kiukweli vvti na D4 ndo current modified features za injini ambazo ziko effective na efficient kwa kila kitu yaani nguvu, mwendo, ulaji wa mafuta na uhimili wa kazi, mi mwenyewe nnayo toyota allex vvti moto wake usipime,

Nami sasa nimeelewa , thanks a lot :)
 
1G fe haina imeme sana kama ilivyo vvti lakini vvti inatumia mafuta kidogo sana ukilinganisha na 1G fe teknolojia hapo ni kupunguza uchafuzi wa mazingira na matumizi kidogo ya mafuta huku ikiacha nguvu ya kutosha keenye gari husika
 
Habari,

Naomba msaada kujua tofauti ya ENgine kati ya 1G-Fe ukilinganisha na VVti kama zote ni CC 2000.

Please naomba msaada maana nahitaji kufanya maamuzi ya haraka.

Ahsanteni sana
Fuata ushauri huu,ukiambiwa ununue simu ya Samsung version yenye antenna na Samsung galaxy S4 utachukua ipi?utachukua yenye antenna ambayo ikiharibika ina mafundi au utachukua galaxy S4 ambayo haina mafundi lakini ni more efficient!tafakari uamuzi ni wako.
 
kwani huko veta hawaoni mabadiliko ya teknolojia waandae mitaala inayokidhi soko?

mimi nitanunua engine ya vvt-i au D4-D common rail zenye matumizi madogo kwenye mafuta na hazina kelele
 
du! mie Cresta GX 100 VVTi engine inanisumbua kiasi, nimebadili engine lkn naona bado mafundi hawaijulia
kwa sasa ipo kwa fundi bado ni tatizo, naomba ushauri hio nyingine (D4-D) ni nzuri zaidi?
 
Jamani ee mimi baada ya kusikia mengi nimenunua engine ya D4 na so far sijaona tatizo gari inafanya kazi sawia kabisa. Sijui huko mbeleni na nimeenda garage kuwauliza mafundi wanasema hamna tatizo lolote na ni miaka 2 sasa nazingatia tu service basi na huduma zingine.
 
Shida wengi wetu tunasikiliyma mafundi tukiamini ndio madaktari wa matatizo ya gari zetu. Lakini tukumbuke,mafundi wengi hawajasoma bali wanatumia uzoefu. Na hata waliosoma,ni wachache huwa wanajiongeza kwenda na mabadiliko ya technology. Sasa,mafundi wengi wakiona kifaa au system ya kisasa hakubali kushindwa. Atajaribu jaribu mradi apate pesa ya kula,mwisho anakuharibia gari na kukwambia aina hii ya kisasa sio nzuri(unategemea aseme vipi). Kwa ufupi VVT-i ndio toleo la karibuni la engine za automatic. Ndio engine inayosifiwa kwa kuunganisha umeme,manual na inteligence-akili. Engine yako imepewa uwezo wa ku reason hata kile unachofanya wewe dereva. Mfano Si kwamba ukikanyaga mafuta tu lazima yote yaende kuchomwa kwenye engine. Mafundi jiongezeni kielimu muende na mabadiliko!
 
Jamani ee mimi baada ya kusikia mengi nimenunua engine ya D4 na so far sijaona tatizo gari inafanya kazi sawia kabisa. Sijui huko mbeleni na nimeenda garage kuwauliza mafundi wanasema hamna tatizo lolote na ni miaka 2 sasa nazingatia tu service basi na huduma zingine.

SAfi sana mkuu hiyo ndio engine ambayo ndio mzungu kaitoa na inasifa kila idara nguvu ,inakula mafuta kidogo sana na nirafiki wa mazingira.
hapo mkuu cha msingi zaidi ya kuzingatia service hakikisha suala la mafuta unazingatia usiweke mafuta ya magumashi yaliyochakachuliwa au machafu na usitumie mafuta mpaka gari inazimika. achana na mambo ya kupuliza air clener mda ukifika badili mpya utaenjoy na hutoijutia engine ya D4
 
kweli zipo vvti lakini ni tofauti saza mpaka kwenye matengenezo spare ila vvt ni bora kuliko 1g fe katika kupaform vvt ipo vzr ila inahitaji uangalizi wa hali ya juu sana
 
Habari,

Naomba msaada kujua tofauti ya ENgine kati ya 1G-Fe ukilinganisha na VVti kama zote ni CC 2000.

Please naomba msaada maana nahitaji kufanya maamuzi ya haraka.

Ahsanteni sana
Naomba nikushauli kitu kimoja ktk maswala ya engine pamoja na specification zake.
Zote hizi ziko sawa na ndio maana zipo sokoni.
Ushauli, unaponunua gari yenye aina ya engine kati ya hizo, jaribu kuomba upewe jarida dogo tu la pms ya injini.
Hili jarida ni la kukuonyesha kipi cha kuangalia au kubadilisha au kureset baada ya masaa kadha, apart from general service ya gari ya kumwaga oil. (Preventive maintenance system )
Kwa kuwa hizi gari zina electronic nyingi sana, mfumo wa electronic nao hufanyiwa service, kitu hiki kwa inchi yetu sijawahi kuona garage zinazo fanya.
Mfano gari za sasa huwa na kifaa sensor ktk mfumo wake wa gesi chafu na hii ndiyo muhimu kwa kuwa ndio inayopeleka ujumbe ktk control system jinsi gani Moshi unavyotoka either sawa au la. Na zina muda wake wa masaa ukifika lzm zinabadilshwa. Kuna yeyote aliyewahi badirisha? Hakuna.
Kwa hiyo tuwe na tabia ya kujua jinsi gani ya kutunza kulingana na manufacture recommendation.
Unaponunua gari hakikisha unachukua maintenance manual,
Tafadhali maintenance manual lzm upewe na lzm wewe mtumiaji uisome.
Workshop manual ya gari huwa hawakupi inabaki kiwandani au inakuwa kwa service agent wao.
Usichanganye kati ya maintenance manual na workshop manual

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom