Naomba msaada wa kikatiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada wa kikatiba

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by adoado, Jul 11, 2010.

 1. a

  adoado Member

  #1
  Jul 11, 2010
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakubwa naomba mnisaidie mantiki ya katiba yetu kuzuia wagombea wasio ridhishwa na matokeo ya urais kupeleka kesi mahakamani ili kupata haki yao.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 11, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Title mbona haiendani na swali lenyewe! Anyway, Ibara ya 41 (7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inasema kama ifuatavyo: "Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake."
  Mantiki yake ni kulinda Kiti cha Rais maana Kiti hicho ni nyeti sana. Sasa kama Rais anaweza tu kuondolewa kirahisi rahisi hivyo na Mahakama nchi itabaki na amani kweli? Hata hivyo naona kama Rais wa Tanzania karibu yuko juu ya Sheria za nchi, ukiondoa mambo machache yaliyoongelewa kwenye Ibara ya 46A ya Katiba ya Mwaka 1977.
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mpendwa Buchanan, Mhhhh, Pamoja na kulinda kiti hapo hapo amenyongwa mwananchi endapo rais ataamua kuingilia mchakato wa uchaguzi kupitia mkurugenzi wa uchaguzi aliyemchangua mwenyewe. Fikiri kwamba katika nchi kumekuwa na hakika kuwa mgombea x kapata kura milioni 10 na mgombe y kapata kura milioni 8 maana hata kama ni uchaguzi matokeo yako wazi na watu wanakuwa nayo. Wakihesabu wanaona idadi ya hakika ni ngapi, kisha mkurugenzi wa uchaguzi bila haya anatangaza kuwa mgombea y kapata kura 10,000,000 na mgombea x kapata kura 8,000,000; mabo yanaisha kihivyo hivyo tu? Hapa mi nadhani ni tatizo!
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jul 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo unafikiri kuwa mantiki ya Ibara ya 41 (7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ni ipi, maana ndio swali la mtoa hoja!
   
 5. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Niliwahi kusikia siku moja kwamba mahakama ikieleza kwamba tangu aingie madaraka rais JK hajawahi kuingilia uhuru wa mahakama
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani ni kuinyonga demokrasia kwa kutumia tu vigezo vya kufikirika upande mmoja. Haiwezekani kwamba kuwe na kutohoji kama ukubaliani na yale ambayo tume imetangaza. Nimekupa mfano hapo juu. Katiba ilitunyonga wapiga kura kwa aina yake.
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Buchanan, kama Rais anaingia madarakani bila ridhaa ya wapiga kura wengi matokeo yake ni chaos. Kumbuka Kenya wananchi wali resist kwa sababu rais alichukuana na jaji mkuu wakaenda viwanja vya Ikulu kwa haraka wakaapa kwa haraka mpaka jamaa akakosea kula kiapo.
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Jul 14, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mimi naelewa kwamba Rais LAZIMA atokane na ridhaa ya wananchi walio wengi, ila nilikuwa naelezea "mantiki" ya Ibara ya 41 (7), bila kujali kwamba Ibara hiyo ni "nzuri" au la!
   
Loading...