Naomba msaada wa damu group O negative kuokoa maisha ya baba yangu

Yale matangazo kuwa damu zipo na ni bure kumbe ni uongo na upotoshaji!
 
Nimesikitika kwa kweli, nilienda kumuona mzee pale hospitali ....kwa kweli nimesikitika!
 
Watu waliochangia damu kwa mgonjwa huyu nimewajulisha wamesikitika sana!
 
group O- ni shida kupatikana sana...hivi icho chama cha wenye hili group sijakiskia??
 
Hii blood group ni shida sana. Isipokuwa kwenye familia yao kuna baadhi walikuwa na group hiyo ila hawajui. Mie pia dada yangu alipata tatizo na akatakiwa kufanyiwa operesheni tatizo likawa damu. Yeye ana B-ve. Tukaambiwa hata tukipata O-ve ni sawa. Tulianza kuhangaika kwa watu kutafuta bila kujua mimi mdogo wake ninayo O-ve kwa sababu wengi wetu hatujui blood group zetu. Baada ya kutafuta sana dr mmoja ndo akauliza kwani hana ndugu? Ndo tukaenda kupima nikapatikana mimi nikamtolea. Haya masuala ya blood group ni ya kurithi hivyo ni vyema watu kupima kujua blood group zao kuokoa maisha ya wenzetu. Namshauri mtoa mada ajitahidi kupima ndugu zao blood group zao ili ikitokea wakati mwingine iwe rahisi kumtambua alierithi kwa baba.

Samahani kwa story ndefu ilhali thread yenyewe ilitolewa kabla hata sijajiunga jf.
 
nimepitia kusoma UZI huu nimedondosha machozi, nakumbuka nilitafuta watu kadhaa, tukakubaliana tufanye ubinadamu (japo alikuwa na hali ngumu kifedha hakuwa tayari kutoza pesa kwa kuokoa uhai wa mtu)
Nilijifunza kitu adimu sana.
 
Una matatizo wewe si bure.
Mdogo wake una O negative........ Dada ana B negative...... Ok hope ni wa baba mkubwa au mama mkubwa lakini sio baba na mama mmoja. Kama ni baba na mama mmoja then mawili either hosp walikosea kupima magroup au uongee na mama vizuri
Hii blood group ni shida sana. Isipokuwa kwenye familia yao kuna baadhi walikuwa na group hiyo ila hawajui. Mie pia dada yangu alipata tatizo na akatakiwa kufanyiwa operesheni tatizo likawa damu. Yeye ana B-ve. Tukaambiwa hata tukipata O-ve ni sawa. Tulianza kuhangaika kwa watu kutafuta bila kujua mimi mdogo wake ninayo O-ve kwa sababu wengi wetu hatujui blood group zetu. Baada ya kutafuta sana dr mmoja ndo akauliza kwani hana ndugu? Ndo tukaenda kupima nikapatikana mimi nikamtolea. Haya masuala ya blood group ni ya kurithi hivyo ni vyema watu kupima kujua blood group zao kuokoa maisha ya wenzetu. Namshauri mtoa mada ajitahidi kupima ndugu zao blood group zao ili ikitokea wakati mwingine iwe rahisi kumtambua alierithi kwa baba.

Samahani kwa story ndefu ilhali thread yenyewe ilitolewa kabla hata sijajiunga jf.
 
nimepitia kusoma UZI huu nimedondosha machozi, nakumbuka nilitafuta watu kadhaa, tukakubaliana tufanye ubinadamu (japo alikuwa na hali ngumu kifedha hakuwa tayari kutoza pesa kwa kuokoa uhai wa mtu)
Nilijifunza kitu adimu sana.
Watu hawana ubinadamu wanawaza pesa tu mpaka yakiwakuta, unaweza juona watu walivyokuwa wanashawishi kuweka pesa mbele ili upate huduma ndio tulipofikia sasa hivi. Lakini kwa yule anayesoma uzi huu ajue tu suala la damu halina mwenyewe likiachwa kuangaliwa kwa minajili ya pesa watu wengii sana tutawapoteza. Immagine unasafiri unapata ajali eneo ambalo hauna ndugu na haujulikani unaenda hosp damu hakuna unafanyaje? Au unafika ukiwa hujitambui na damu ipo ila watoa huduma wameshazoea damu haitoki bila pesa kifuatacho ni nini? Una pesa zako lakini wachangiaji wa hiari tumegoma kuchangia kwa kuwa tukichangia inauzwa utanunua wapi? Umeenda na mke wako hosp kujifungua usiku wa manane anahitaji damu ndugu zako hawawezi kupatikana na damu hakuna hosp unafanya nn?

Nadhani ni jukumu letu sote kuchangia damu kwa hiari na kama huna sifa za kuchangia at least hamasisha watu wachangie damu kwa hiari.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom