Naomba msaada tatizo la kusinzia darasani

Habari wanaJF wote,

Nina umri wa miaka 19 npo kidato cha tano. Nipo hapa kuomba ushauri na msaada kuhusu tatizo langu la kusinzia darasani hasa mwalimu anapokua anafundisha, hasa mida ya mchana hivi ghafla usingizi mzito unanishika na hua siwez kujizuia mpaka mwalimu au rafiki yangu anishitue, hata hivyo tatizo la usingizi huendelea kunikumba........

Je ni tatizo la kiafya? Au ni nini chanzo chake japo usiku hua nalala muda wa kutosha tu... Msaada tafadhal mana hii hali nimeichoka na siihitaji iendelee kunitesa Mana mwisho wa kipindi usingizi huisha na hua naamulia patupu kwa kile mwl alichofundisha.

mhh hiyo sura hiyo kwanini usisinzie
 
mbona hao ndio wanachochea hizo nguvu za giza.
Sio kweli kaka ila wanazingiziwa sana, mimi sina nguvu yoyote ya giza lakini nimewahi kuhudumu sana kwenye shule za sekondari na wanafunzi kibao walikuwa wanafunguliwa saaana , ninajua kwasababu nina shuuhuda, mambo niliyokuwa nakutana nayo kaka sio ya kawaida, na kuna baadhi ya shule zina wachungaji kabisa, lakini nilipokuwa nikifika kwa huduma hata hao wachungaji walikuwa wananifikiria kama nina nguvu za giza.
 
Usisumbuke sio tatizo kubwa sana na ukahofu kwamba litakufanya ufeli. Watu wenye kusinzia darasani wakipata muda ambao hawasinzii akili yao ina uwezo mkubwa sana ya kuelewa na kutunza kumbukumbu hivyo usiwe na hofu sana bado una nafasi nzuri sana ya kufaulu kuliko hata wasiosinzia darasani

ebwana mkuu asante sana.. Nimekuelewa vema
 
Jaribu kuwa na lengo madhubuti kwa kila kipindi kabla mwalimu hajaingia darasani.
Mfano, natamani kujua ............ na leo ndio mwalimu atafundisha, so ile ....... niliokuwa naishangaa leo lazima nikitoka niwe nimeipata vizuri, asipozungumzia nitamuuliza.
tayarisha maswali kama 3 ya kumuuliza mwalimu, au unaweza kuyapata anapoongea.

hapo ni baada ya kumuona daktari na kukujulisha huna ugonjwa kautisha.
Wengi husinzia pale wanaposhindwa kupata relevancy ya kinachozungumzwa na wao. au malengo yao. inawezekana bado hujajua hivyo vipindi vinauhusiano gani na malengo yako makubwa, nadhani unaviunganisha na lengo lakufaulu mtihani tu.

asante sana mkuu hapo nimekuelewa vema
 
Mwenzio nilipokuwa kidato cha NNE nilikwenda hospitali tumbi. Doctor alianza kupekuwa madocument kwani hajapambana mda mrefu na tatizo hilo. Alukutana na Maelezo furani. Akanishauri kupima kiwango cha sukari. Kwangu aliona sukari iko sawa lakini huenda kwako ikawa ndiyo tatizo. Alinipa dawa na kunitaka nirudi tena japo sikurudi.
Mzizi mkavu angekusaidia ila sikugizi anashinda jamiifotos
 
enzi zile nasoma nilipatwa na huu ugonjwa nikagundua dawa yake ni kukaa siti ya mbele kabisa, tabia hii ilinisaidia mpaka nilipokuwa chuo niliendelea kukaa mbele kabisa.
Jenga mazoea ya kuuliza maswali na kujibu jaribu hata kama hujui wakati wa kipindi itakusaidia kuongeza concentration na usingizi utaondoka.
 
Kaa mbele yaani utizamane na mwalimu pia usaidie kufuta ubao jitahidi kuwa unauliza maswali hata kama ni pumba na pia kujibu maswali class we jibu tuu si unajua kuna ile dhana ya there is no right or wrong answer na wote mko kujifunza

Ushauri mzuri. Nami nilikuwaga na hili tatizo. Vipindi vya mchana ilikuwaga shughuli, mara nyingi hutokea kama hauna interest na kipindi au mwalimu. Ulizaga maswali na ukae mbele, ukishiriki kisawa sawa ktk kipindi.
 
Habari wanaJF wote,

Nina umri wa miaka 19 npo kidato cha tano. Nipo hapa kuomba ushauri na msaada kuhusu tatizo langu la kusinzia darasani hasa mwalimu anapokua anafundisha, hasa mida ya mchana hivi ghafla usingizi mzito unanishika na hua siwez kujizuia mpaka mwalimu au rafiki yangu anishitue, hata hivyo tatizo la usingizi huendelea kunikumba........

Je ni tatizo la kiafya? Au ni nini chanzo chake japo usiku hua nalala muda wa kutosha tu... Msaada tafadhal mana hii hali nimeichoka na siihitaji iendelee kunitesa Mana mwisho wa kipindi usingizi huisha na hua naamulia patupu kwa kile mwl alichofundisha.
Kanunuwe shubiri nyekundu uisage upate unga wake nusu kijiko cha chai kisha unaitia kwenye maji unakunywa mara 2 kwa siku asubuhi na usiku kwa muda wa siku3 utapona. Hiyo shubiri ni chungu uvumilie ndio dawa inapatikana kwenye maduka ya dawa za kisuna Kama upo mjini Dares-Salaam nenda karibu na Soko Kuu la Kariakoo uliza Maduka ya dawa za kisuna utapata hiyo dawa. Angalia picha hapo.
 
Attachments

  • shubiri.jpg
    shubiri.jpg
    25.6 KB · Views: 178
punguza kula viporo mdogo wangu maana viporo husababisha mtu kusinzia sana!
 
Habari wanaJF wote,

Nina umri wa miaka 19 npo kidato cha tano. Nipo hapa kuomba ushauri na msaada kuhusu tatizo langu la kusinzia darasani hasa mwalimu anapokua anafundisha, hasa mida ya mchana hivi ghafla usingizi mzito unanishika na hua siwez kujizuia mpaka mwalimu au rafiki yangu anishitue, hata hivyo tatizo la usingizi huendelea kunikumba........

Je ni tatizo la kiafya? Au ni nini chanzo chake japo usiku hua nalala muda wa kutosha tu... Msaada tafadhal mana hii hali nimeichoka na siihitaji iendelee kunitesa Mana mwisho wa kipindi usingizi huisha na hua naamulia patupu kwa kile mwl alichofundisha.

Pole sana.

Mimi kilichonisaidia nilipokuwa na shida kama hiyo ni kutumia a fortified B-Complex vitamins. Inasaidia sana kufanya ubongo wako uwe alert na u-concentrate.

Mimi sio daktari wa binaaamu. Ninachokueleza ni experience yangu na sio medical advice.
 
Back
Top Bottom