Naomba msaada slow laptop

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,700
1,415
Laptop yangu ya Toshiba satellite kwa wiki mbili sasa imekua slow sana kufungua webpage nayotaka nami sio mtaalamu wa mambo haya sijui mnanishauri nifanye nini? Haikuwa hivi mwanzo nipo Uhuruone wifi ambayo speed na signal strength yake ni nzuri.
 
Kwakuwa huna utaalam na masuala haya nashindwa kukusaidia maana kila ntakalokuuliza utaliona limeandikwa kiufundi zaidi... Nilitaka kujua unatumia antivirus gani, unafanya cleanup ya pc yako (virus & memory) kila baada ya muda gani?

Internet una-browse kwa kutumia browser gani? Kilicho slow ni pc au internet connection? Very sorry, mengine nashindwa kukuuliza
 
Kwa kuongeza Je umekuwapo na hiyo laptop kwa muda gani? tunaposubiria majibu nenda kwanye webpage click Tools -> Internet Options ->Select General Tab then under Browsing History click delete button halafu angalia kama kutakuwa na mabadiriko yoyote. Hii process ipo valid kama unatumia Windows Internet Explorer. Kwa browser zingine tofauti itakuwapo lakini si vile.
 
Natumia AVG antivirus nafanya cleanup kila wiki,ya memory nimefanya sasa hivi baada ya ushauri wa Juakali na browse na Mozzilla Firefox na mara moja moja Explorer na Google chrome,kilicho slow naona pc connection natumia Uhuruone ambayo speed huwa 1-54 Mbps na signal strength yao nzuri.
 
Kwa kuongeza Je umekuwapo na hiyo laptop kwa muda gani? tunaposubiria majibu nenda kwanye webpage click Tools -> Internet Options ->Select General Tab then under Browsing History click delete button halafu angalia kama kutakuwa na mabadiriko yoyote. Hii process ipo valid kama unatumia Windows Internet Explorer. Kwa browser zingine tofauti itakuwapo lakini si vile.

Asante mkuu nimefuta browsing history,nimekuwa na laptop hii mwaka mmoja na kabla ya hapo ilitumiwa na ndugu yangu.
 
Laptop yangu ya Toshiba satellite kwa wiki mbili sasa imekua slow sana kufungua webpage nayotaka nami sio mtaalamu wa mambo haya sijui mnanishauri nifanye nini? Haikuwa hivi mwanzo nipo Uhuruone wifi ambayo speed na signal strength yake ni nzuri.
Mkuu Ha ha hiyo naona imejaa zile picha zetu kwi kwi...Just kidding!.
 
Kama utakuwa jasiri, ACHANA NA WINDOWS, tumia Ubuntu. Niko tayari kukuwekea hiyo Operating System, kwani inatolewa Bure (huna haja ya kutafuta pirated keys), na daima hutapata matatizo ya virus, spyware au trojans! Ni very stable, haisumbui, na utapata shida ku-crash na kupoteza data zako. Kama ni browsing, inakuja na Mozilla Firefox na software nyingine kibao. Kwa upande wa speed, ni kiboko. Laptop yako ita-boot at least 400% faster kuliko Windows. Software zote unatakazohitaji zinapatikana online. Kwa mfano, OpenOfficeORG ambayo ndiyo Office Suite, iliyotengenezwa na Sun Microsystems, inatolewa bure, na imewekwa tayari kwenye DISTRIBUTION (soma DISTRO) ya Ubuntu. Unaweza kuandika files zako, ukasave kwenye .DOC format, na mtu anayetumia MS Office akazisoma pia. Hata .XLS files, na presentation (inaitwa IMPRESS) ni nzuri ZAIDI kuliko PowerPoint.

Nitumie PM tuwasiliane.

./Mwana wa Haki
 
P.S. Kama una nafasi ya kutosha kwenye laptop yako, unaweza kuweka Windows na Ubuntu pamoja kwenye laptop, ukawa unachagua OS ya kuingia unapo-boot.
 
Kama utakuwa jasiri, ACHANA NA WINDOWS, tumia Ubuntu. Niko tayari kukuwekea hiyo Operating System, kwani inatolewa Bure (huna haja ya kutafuta pirated keys), na daima hutapata matatizo ya virus, spyware au trojans! Ni very stable, haisumbui, na utapata shida ku-crash na kupoteza data zako. Kama ni browsing, inakuja na Mozilla Firefox na software nyingine kibao. Kwa upande wa speed, ni kiboko. Laptop yako ita-boot at least 400% faster kuliko Windows. Software zote unatakazohitaji zinapatikana online. Kwa mfano, OpenOfficeORG ambayo ndiyo Office Suite, iliyotengenezwa na Sun Microsystems, inatolewa bure, na imewekwa tayari kwenye DISTRIBUTION (soma DISTRO) ya Ubuntu. Unaweza kuandika files zako, ukasave kwenye .DOC format, na mtu anayetumia MS Office akazisoma pia. Hata .XLS files, na presentation (inaitwa IMPRESS) ni nzuri ZAIDI kuliko PowerPoint.

Nitumie PM tuwasiliane.

./Mwana wa Haki
Hapo kwenye bold unaongelea windows 3.1?
Harafu ushauri wa kuhamia ubuntu inategemea sana system yako unatumia kwa makusudi gani kwani kuna millions ya applications ambazo hazitarun kwenye ubuntu especially application specific ambazo watengeneza wanatarget market kubwa ya PC.
 
... tumia Ubuntu. Niko tayari kukuwekea hiyo Operating System, kwani inatolewa Bure...

Nitumie PM tuwasiliane.
unamshauri mtu apachike Ubuntu kama hata ku install ni mpaka mkutane umuwekea, ina maana itamsumbua. ..unless, obviously, unataka kum-kula, wakati kitu yenyewe mwenyewe umesema ya bure... tuwasiliane?
Kilicho slow ni pc au internet connection? Very sorry, mengine nashindwa kukuuliza
Akijaribu ku browse ngoma inafunguka slow, yeye atajuaje whether ni computer au browser?

Na kama mganga angekuwa anakwambia "oooh, very sorry nashindwa kukuuliza maswali maana utaona ya kitaalam sana" tungepona kweli? Mafundi wetu bana
 
Laptop yangu ya Toshiba satellite kwa wiki mbili sasa imekua slow sana kufungua webpage nayotaka nami sio mtaalamu wa mambo haya sijui mnanishauri nifanye nini? Haikuwa hivi mwanzo nipo Uhuruone wifi ambayo speed na signal strength yake ni nzuri.

Kwanza naomba quantitative estiatamion ya hiyo slowness. kwenye adress bar ukiweka google.com alafu uki kong'oli Enter inachukua sekunde au dk ngapi kabla haijaja page ya google.com, Jamiiforums.com na Webopedia.com. jaribu kuhesabu response time ya kila moja toka umebonyeza enter mpaka inapokuletea page kamili.-Itasaidia watalaamu kujua how slow your comnection is

speed Nina wasi wasi speed unayosoma sio ya uhuruone bali ni maximum speed ya wireless card ya kompyuta yako. kujua speed halisi wakati unajaribu coconnet kwenye internet , Kama laptop yako XP nenda kwenye Wireless Connection Status Angalia diff kati ya packets sent na packet received . Vile Vile quantify hizo speed unazosema ni nzuri.

Leta hizo quantitative data naweza kujaribu kukupa ushauri
NB
kwa haraka haraka tatizo la hili sio la OS kwa hiyo halihusiani na windows wala ubuntu. Tatizo linaweza kuwa ni la hardware hasa Wireless Card au ni la Connection (ISP)
 
Ninavyomwelewa jamaa ni kwamba computer yake ilikuwa nzuri kwa mwaka mzima, imekuja kukorofisha wiki mbili tatu zilizopita.
Inawezekana kabida kuwa katika pitapita online ukapitia site mbaya ikainstall vt ndani ya lapton yako na wakati mwingine siyo rahisi hata kwa antivirus kugutukia. Sasa njia moja wapo ya kutatua shida kama hii ni kutumia "System Restore" Nenda Start->All Programs ->Accessories -> System Tools -> System Restore halafu chagua tarehe ya nyuma pale system yako ilikuwa ina-run vizuri. Click next harafu iache system ifanye mambo yake ikiwa tayari itareboot. Jaribu hiyo wakati tunaendelea kukuna vichwa:confused2:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom