Naomba msaada ndugu zangu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada ndugu zangu.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by 4 PRINCE, May 23, 2011.

 1. 4

  4 PRINCE Senior Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna dada yangu amenijia kutaka ushauri,amegundua kuwa mume wake ametembea na rafiki zake wawili,house girl wake,wifi yake yaani mke wa kaka yake,mwanaume huyu katembea pia na dada zake wa kuzaliwa nae,wawili.majirani zao zaidi ya wanne.

  pia inasemekana huko nyuma kabla hajamuoa huyu dada,alikuwa na mke mwingine,ambapo alitembea na mama mzazi na dada wa huyo mke,pia aliwahi kufanya mapenzi na kichaa.amejaribu kufanya hesabu wanawake waliozini ni mume wake ni zaid ya 200.

  Na mume huyu amekiri mwenyewe kwa kinywa chake baada ya kufanyiwa maombi.sasa anaomba msamaha akidai kuwa kulikuwa na nguvu iliyokuwa inamsukuma kufanya mambo hayo.maana mbali ya kufanya mapenzi na watu wote hao,pia alikuwa na tabia ya kujichua kwa kutumia picha za wanawake aliokuwa akikutana nao njiani,au wale waliokuwa wanamkataa,ingawa anadai alikuwa hakataliwi akimtaka mwanamke.wamo wake za watu wengi tu.

  Huyu dada ananiuliza je amsamehe?au afanyeje?maana analia na kusema alikuwa hajitambui.Nawaomba ndugu zangu,nisaidieani,nimshauri vipi?
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mi sielewi, anataka amsamehe nini tena kama 'amekwishaombewa' na kukiri?
  Yaishe, alikuwa na pepo na limeshatoka!
   
 3. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Hayo mambo yashaisha waangalie mbele tu hakuna kurudi nyuma
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aisee....maajabu ya dunia hii ni mengi kweli!Too bad kila tunalokosea tunamsingizia shetani wa watu na mapepo utadhani hua yanawashika watu mkono kuwapeleka kusiko!

  Kuhusu kama amsamehe au lah inabidi uwe ni uamuzi binafsi bila uchochezi kutoka kwa mtu yeyote maana leo na kesho akija kutembea na mwanae lawama zisije zikamwendea aliyeshawishi msamaha utolewe!Dada afikirie ni kiasi gani anampenda mumewe...kama anamwamini kuhusu kubadilika na ni kwa kiasi ganu yuko tayari kukutana na mengine ya ajabu zaidi huko mbeleni ikiwa mume hajabadilika ndo ajue kama amsamehe na kuendelea nae au amsamehe na kusonga mbele!!
  Pole yake!
   
 5. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,807
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  Duh! Dunia ina mijimambo eehe
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  amsamehe tena kwa moyo mmoja ila amwambie kuwa one mistake kwisha habari yake.na kweli akirudia tu hakuna kumsamehe tena, watu kama hawa ni kama kina klorokwini (makatuni) na wana heshima zao high konvisingi pawa
   
 7. k

  kisukari JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  thank you haitoshi lizzy ila nakupa mia kwa mia.kwa mtazamo wangu,umeandika point
   
 8. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,711
  Trophy Points: 280
  huwezi kuambiwa na mtu kumsamehe isipokuwa wewe mwenyewe na moyo wako na pia uwe umeridhika na mabadiliko ya mumeo.
  endelea kufwatilia tabia yake kwa karibu kujua kama ameachana na tabia mbaya aliyonayo..............inawezekana ameona tabia yake imegundulika sasa ameamua kuzuga kubadilika
   
 9. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,164
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  Naamini ktk uwepo wa MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI. Aliye weka dini hakika alikuwa na akili sana na hadi sasa tunaona anavo endelea kuiamonaizi jamii, hebu angalia mtu anavo mkosea mwenzake tena mimakosa mikubwa mikubwa tuu alafu wanakutanishwa na kupatanishwa ktk misingi ya dini, mkosaji anawekwa kando na SHETANI NA USHETANI WAKE anasimamishwa na kubeba mimakosa yoooooooote ya mkosaji akiachwa! basi na mkosewaji kwa hisia zilizojengwa katika imani hiyo humchukia shetani na kuungana na mkosaji nao wakizidi kumshutum shetani! Unajua YESU atarudi kukomesha dhambi OLE WAKO AKUKUTE NAYO! kwan yeye shida yake ni dhambi tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu ndo alo ilenga
   
 10. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  amsamehe tu.lakini huyo jamaa kawafaidi wote hao!?inatosha,inabidi sasa atulie angalie ndoa yake coz wazuri hawaishi.
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Asante kiSugar....hehhee!
   
 12. Nemo

  Nemo JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 661
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 80
  4 PRINCE
  Kulikuwa na nguvu................................. Hajitambui............................. Like really??
  When will women learn that enough is enough !?? In my opinion husbands lacking consequences in this society of ours for their disgusting actions such as above is what encourages these men kuendelea kufanya upuuzi kama huu!!!!
   
 13. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kuna wanawake pia wa jinsi hiyo usisahau! Nilishashuhudia ugomvi mtaani ambapo wanawake wawili walikuwa wanapigana. Walipoulizwa kisa mmoja wao akasema: "Yeye alijifanya mwanamke na nusu kunichukulia mume wangu, nami nimemchukulia wake, bwana'ake wa pembeni, kaka yake na shemeji yake ili akome!"
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Hivi huyo mama mkwe anaenda kutembea na mkwe ni akili?Na hao dada za mke ah!,anyway,mwambie kuwa aamue mwenyewe kama amsamehe au la,mambo mengine mpaka kinyaa!
   
 15. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Binadamu hivi kusamehe na kusahau vinaenda pamoja ,kusamehe ni muhimu kwa afya ya moyo wake ,kusahau mtu ame f.a.c.k wote hao.anauwezo wa kusahau , kama atakuwa akimwona then anaona umalaya wake ,msamaha utakuwa cover tu sio uhalisia!
   
 16. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wasiwasi wangu ni kwamba ka huyo jamaa alishawahi kula kichaa, dada zake, mamamkwe hata mamake mzazi hatachelewa, tusibase sana kumlaumu shetani.
  Kuhusu msamaha huyo dada aamue mwenyewe kwa kuzingatia mazingira alivofanya makosa, na the way anavoomba msamaha. Mi sitoi jibu.
   
 17. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jamani hapo pagumu sana, maana jamaa amepita kiwango!!! mmh sijui tumpeleke Samunge....???? dada kaza moyo majaribu ya dunia haya
   
 18. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Huyu alizaliwa duniani kimakosa au? maana hata haridhiki kabisa hadi kujichua jamani?
   
 19. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jamaa anahitaji maombi, maana anaweza hata kuwageuka binti zake!!!
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  May 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  kivuli hakina rangi
   
Loading...