Naomba Msaada kuhusu kuingia Mkataba Ardhi Kimakosa.

Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,946
3,685
Nimefatwa na Mama mmoja asiyejua kusoma lakini yupo kwenye ndoa.
Ameishi na mumewe kwa zaidi ya Miaka Kumi lakini hakubahatika kupata Mtoto.
Mume wake kamshawishi wamrithishe kijana mmoja Mali zao pindi watakapofariki.Inasemekana kijana huyo amejikomiti kutoa huduma zote kwa hao wazee kwa kipindi chote watakachokuwa hai.
Huyo mama anacholalamika ni kwamba hapati huduma zozote kutoka kwa huyo kijana,isipokuwa Mara chache humpa mume wake pesa ambazo huzitumia apendavyo pekee.Yeye anaishi kwa kufanya vibarua,hivyo anahisi mume wake na Huyo Kijana walishirikiana kumtapeli ili asaini hayo makubaliano.
Ameniomba ushauri jinsi ya kuvunja mkataba huo.
Mbaya zaidi hana hata Nakala ya hayo Makubaliano.
Naombeni ushauri wenu hasa ukizingatia Mkataba huu umeshadumu kwa takribani Mwaka sasa.
 
hayo makubaliano yanaukakasi lakini ngoja niguse haya machache
1. km wamiliki wa mali ni wawili na wanataka kuandaa wosia kwa pamoja hiyo itakuwa ni joint will na inaweza kubadilishwa contents zake ikiwa wausia wote bado wako hai
2.ikiwa mtoa wosia alifanya hivyo pasipo kujua nini afanyacho ie. bila hiari yake mwenyewe basi wosia huo ni batili
3.hata km wosia ni halali mali ya mtoa wosia haiwezi kuathiriwa na wosia husika ikiwa mtoa wosia angali hai
 
Back
Top Bottom