Naomba msaada kuhusu Internet kwenye Samsung Galaxy Note 3 Neo

Jan 22, 2014
65
38
Wakuu naomba msaada wenu,

Mimi na ndugu yangu tumenunua Samsung Galaxy Note 3 Neo na tumekuwa tukizitumia ikiwa ni nimiezi 3 sasa. Hizi simu zina uwezo wa kubeba simcards 2, mimi natumia mtandao pendwa wa Tigo pekee na ndugu yangu ameweka simcards za Voda na Airtel.

Tatizo linalokuja ni kwamba kila tunaponunua internet bundles hatupati kabisa network ila tunapoamua kutumia WiFi basi zinafanya kazi vizuri tu na mtandao unakamata.

Je kuna mahali tumekosea settings? Naomba msaada wenu maana najua kuna watu ni wazuri sana kwenye vitu kama hivi.
 
Samsung Galaxy Note 3 zina double line?sijawahi kusikia!

Mkuu ni Samsung Galaxy Note 3 Neo...yaani neno "Neo" limeongezwa ili kuitofautisha na hiyo Note 3 uliyoitaja. Kwa zinavyoonekana kwa nje zipo sawa ila hii Neo ni ndogo kidogo na ndizo zenye double lines.
 
Back
Top Bottom