Naomba msaada kilowatts 2.5 ni sawa na kva ngapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada kilowatts 2.5 ni sawa na kva ngapi?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by mgange hussein, Oct 18, 2012.

 1. mgange hussein

  mgange hussein Senior Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nataka kununua generator,vitu ninavyotumia nyumbani jumla ni kilowatts 2.5 sasa nichukue generator ya kva ngapi.Nataka generator ndogo ya wastani itakayofanana na uwezo wa vitu vyangu.Pia naomba kujua maana ya KVA.
   
 2. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  KVA = kilo volts ampere. Hazina tofauti sana na KW kama unatumia 2.5 KW nunua generator ya 2.5 kVa
   
 3. Jaramba

  Jaramba Member

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ki uhandisi zaidi iko namna hii,
  KVA = Kilo Voltage Ampere
  KW = Kilo Watt
  Watt= Voltage (V) * Ampere (A) i.e W= VA

  Kwa ufupi KVA ni sawa na KW ni namna ya rating tu ila kitu kile kile.
  Kama matumizi yako ni 2.5 KW ni vizuri ukanunua generator yenye ukubwa zaidi ya 2.5 KVA kwa sababu ya matumizi ya baadae yanaweza kuongezeka so ni vzr uka-focus future usage pia.
   
 4. W

  Wanzuki Senior Member

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni sawa KVA = Kilo Volt-Ampere, lakini sio sawa na KW (KiloWatts). Kwa machine kama generator (ina resistors, capacitors na inductors), KVA rating yake sio sawa na KW. Katika hali kama hii KVA huwa ni kubwa kidogo kuliko KW. Inabidi KW kugawanya na factor fulani (power factor) ili kupata KVA.
  KVA = KW/Power Factor
  Kwa kesi yako, KVA = 2.5/Power factor. Hii power factor inategemea tofauti ya 'phase' kati ya current na voltage kwa system husika. Kwa kukadiria huwa inatumika 0.8

  Hivyo, utapata: Generator yako iwe angalau 2.5/0.8 = 3.1 KVA. Hivyo ni vizuri ukanunua generator ya kati ya 3.2 - 3.5KVA itakufaa.
   
 5. mujungu

  mujungu Senior Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mkuu hesabu za 3.5kva zimetulia.
   
 6. Loyal_Merchant

  Loyal_Merchant JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 589
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Alichosema wanzuki ni sahihi.
  Tecnically katika umeme kuna kitu kinaitwa load. katika umeme load ni kifaa chochote katika mfumo wa umeme ambacho hubadili umeme kwa maana volts na amperes tunazoozijua kwenda katika nishati fulani i.e mwanga, mekanika, sauti n.k.

  Kuna load za aina tatu,
  1. resistive
  2. inductive
  3. capacitive.

  katika mfumo wa umeme wa D.C unaweza ukasema directly kwamba kizio cha watts ni sawa na kizio cha volt-ampere. Ila katika mfumo wa umeme wa A.C haiko hivyo kwani hizi loads za aina mbili i.e (inductive na capacitive) huwa zinaathiriwa na mfumo huu kwani volt na ampere huwa vinakuwa havipo katika phase moja kwa maana either voltage inai-lead current ama vice versa. Hivyo basi kwa mfumo huu wa AC kuna kitu kinaitwa power factor(P.F) ambapo unaweza sema kwamba power factor ni ratio ya real power inayoenda katika load na apparent power inayozunguka katika mfumo huo wa umeme na kimahesabu

  P.F = cos (angle difference btw V and A)
  KVA * Power Factor = KW

  Ni ngumu sana na practically hakuna electrical system ambayo total load yake ni pure resistive. Na commonly power factor huchukuliwa kama 0.8 kwa system za kawaida, 2.5Kw/0.8 = 3.1Kva Hivyo basi kwa mahitaji yako kama alivyosema wanzuki utahitaji jenereta ya 3.1Kva mpaka 3.5Kva
   
 7. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Correct answer!!
   
 8. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,639
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Yeah, you went to study, not only to read. You're right
   
 9. Loyal_Merchant

  Loyal_Merchant JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 589
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Alichosema wanzuki ni sahihi.
  Tecnically katika umeme kuna kitu kinaitwa load. katika umeme load ni kifaa chochote katika mfumo wa umeme ambacho hubadili umeme kwa maana volts na amperes tunazoozijua kwenda katika nishati fulani i.e mwanga, mekanika, sauti n.k.

  Kuna load za aina tatu,
  1. resistive
  2. inductive
  3. capacitive.

  katika mfumo wa umeme wa D.C unaweza ukasema directly kwamba kizio cha watts ni sawa na kizio cha volt-ampere. Ila katika mfumo wa umeme wa A.C haiko hivyo kwani hizi loads za aina mbili i.e (inductive na capacitive) huwa zinaathiriwa na mfumo huu kwani volt na ampere huwa vinakuwa havipo katika phase moja kwa maana either voltage inai-lead current ama vice versa. Hivyo basi kwa mfumo huu wa AC kuna kitu kinaitwa power factor(P.F) ambapo unaweza sema kwamba power factor ni ratio ya real power inayoenda katika load na apparent power inayozunguka katika mfumo huo wa umeme na kimahesabu

  P.F = cos (angle difference btw V and A)
  KVA * Power Factor = KW

  Ni ngumu sana na practically hakuna electrical system ambayo total load yake ni pure resistive. Na commonly power factor huchukuliwa kama 0.8 kwa system za kawaida, 2.5Kw/0.8 = 3.1Kva Hivyo basi kwa mahitaji yako kama alivyosema wanzuki utahitaji jenereta ya 3.1Kva mpaka 3.5Kva
   
 10. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Naam, hii ndiyo Jamii Forum bwana!
   
 11. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,655
  Likes Received: 3,307
  Trophy Points: 280
  Nimelipenda sana somo hili
   
 12. mgange hussein

  mgange hussein Senior Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nashukuru sana wanajamii kwa somo zuri sana.Amani iwe kwenu.
   
Loading...