mkuu kama una data zote weka hapa, hao wanasheria watapata hapa pia, yani moyo wng una mzgo mkubwa wa kuombea ili jambo, mungu awaumbue,achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe.
Kijana leo pole sana kwa kuubebesha moyo wako kitu kizito, kuwa makini usije ukatobolewa na kitu chenye ncha kali. Napata faraja sana kuona jinsi wanaCDM, walivyojivika uhusika wa hili suala. Inaonyesha ni kiasi gani wanamapenzi ya dhati kwa chama chao. Ni kweli hili suala linatuumiza sana vichwa ila angalau sasa upepo umetulia baada ya kupata information kutoka kona mbalimbali zinazoashiria kuwa ushindi utapatikana na ukweli utabainika. Nafurahishwa pia na ujasili ulioonyeshwa na manahodha wetu, katika kutake control ya hali ya mambo/hili dhoruba-Peeeeeeeeeeeeoooopleeee's...............................
Wapo vijana wa IT waliokwisha tuweka wazi kuwa ni fake kwa takwimu/data, wapo hawa sasa wanaoweza kutupeleka hadi kwenye platform waliyoigizia na wapo waliotuletea email ya wahusika wakipongezana kwa kazi nzito na yaziada waliyoifanya kufanikisha hili. Naomba nitambue uwepo wa vijana hawa na binafsi nawashukuru sana.
Aidha, ushiriki wa maccm hasa wale viongozi wa chama katika suala hili, umekuwa hafifu sana jambo linaloashiria hii ishu wameifanya kwa pupa.Tuwe na moyo wasubra, nadhan kesho mchakato wa ukweli kuwa hadarani utaanza pale Kisutu.
Kitu ambacho nadhan maCCM hawafahamu ni kwamba, wasiopenda mwenendo wa hali ya mambo katika Serikali ya CCM sio tu wale waliokuwa mtaani-wasio na ajira au wanachadema. Kuchukiwa kwa CCM na serikali yake hakutokani na mapenzi ya watu kwa chadema. Serikali ya ccm itambue kuwa kuchukiwa yake kunatokana na mambo yanayofanywa na serikali hii kama kulinda na kukumbatia mafisadi,utawala wa kichief, kuficha wauaji, kutusababishia umaskin wa kutupwa na kusababisha kukosekana kwa huduma muhimu kwa wananchi ilihali watu wachache pale juu tunaona wakijineemesha kupita kiasi.
Wakina Nape, Mwigulu na wengine mnayoipenda CCM yenu, hebu tumieni nguvu nyingi kurekebisha hayo niliyoyataja hapo juu badala ya kufanya Propaganda za kitoto. Hata mkikiua chadema leo hii, bado haina maana kuwa wananchi watakipenda chama chenu. Mapenzi kwa chadema ni dalili tu ya Tatizo, tibuni kwanza Tatizo lenyewe, msiangaike kupambana na dalili.
Hata mkiue CDM leo hii tutakuwa radhi kuingia chama kipya kuliko kuja CCM, mbona Kenya wakina Uhuru NA Rutto wameshinda kwa kuokoteza watu via UHURUTO-Jubilee??Mnadhani ni kwanini???Juweni tu hapo mtakuwa bado hamjafanya kitu. Nchi hii sasa hiv wananchi wameelimika-japo kwa magumashi, na wengi wa wapigakura ni wale waliozaliwa ndani ya mfumo wa vyama vingi. Hili lingewapa signal on how to operate, sio mnaendaenda tu kwa nguvu za giza na nguvu za ndum!!