saronga
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 909
- 218
Baadhi ya wagonjwa wa UKIMWI wana kasumba ya kutokubali kwamba wanaumwa Ukimwi, na huu ndio huwa mwanzo wa mwisho wao, maana bora wangekubali wakanywa dawa za kurefusha maisha wangeweza kuishi muda kidogo kulinganisha na juhudi zao za kukataa kwamba wameathirika.
Ndivyo ambavyo chama nilichodhani kingekuwa chama mbadala ya CCM iliyochoka kingekuwa, yaani CHADEMA. Bahati mbaya sana Chadema kama mgonjwa wa UKimwi asiyetaka kukubali kwamba ameathirika badala yake anabaki kuamini kuwa KAROGWA ndio mwanzo wa mwisho wa Chadema!
Hata kama viongozi wa Chama hichi walikimbia shule wengi na wengine shule zao za magumashi ,inahitaji degree ngapi kujifunza kukubali ukweli hata kama unauma? Ugonjwa huu wa kukataa kwamba unaumwa wakati unaumwa na kudhani unarogwa utakizika Chama hichi kilichoanza kuonyesha matumaini...na hapa CCM na wapambe wao watakuwa wamefanikiwa sana.
Hivi inahitaji degree ngapi kujua kuwa Rwakatare ambaye siasa zake za upinzani alianzia CUF na wakati huo CUF ilikuwa na tabia zinazoonekana leo CHADEMA? Wakati CUF ikiwa na Rwakatare ndo ilikuwa chanzo cha vurugu za kisiasa nchini,mara kuingiza visu, mara majambia, mara maandamano, mara watu kuuawa na wengine kupoteza viungo vya miili yao!! Sasa Rwakatare huyuhuyu yuko Chadema leo, Chadema wameiga tabia zilezile zilizowamaliza CUF na wakadhani Chadema wao watakuwa na muujiza wa kuishi.
Dawa hapa nikujua mmeteleza na kuamka sio unateleza unabaki chini unalalamika!!
Acha ujinga wewe, CUF haikuuwawa na Lwakatare, imejiua yenyewe baada ya kukubali ndoa na maccm. Soon ukweli utawekwa hadharani kama ilivyokuwa kwenye issue ya Dr ulimboka. Hebu naomba unikumbushe hivi yule chizi mkenya kesi yake imeshafikishwa mahakamani, au ndo mlituchezea picha halafu mkampatia malipo yake ili apotee? manake sijamsikia tena hata siku moja kupanda kizimbani, au ndo mnataka kuizima kwa hii video feki ya Lwakatare. Vipi rama wa magogoni mbona nayeye ametajwa sana na Dr ulimboka pamoja na rafiki yake Deo, lakini hadi leo si Deo wala rama wala Dr Ulimboka aliyeitwa polisi kusaidia kwenye hilo suala, lakini polisi wameona hili la lwakatare la kwenye mitandao ya kijamii ndo la kushikia bango. Kama mlitegemea mtaivunja nguvu chadema kwa vijipropaganda vya kitoto kama hiki mmenoa, jaribuni pengine. Na kwa taarifa yako tu mgonjwa wa UKIMWI hapa ni maccm ambao wamepatiwa tiba mbadala lakini wamegoma kuimeza, kifo kinawakaribia sasa ndo maana wanatafuta pa kuponea. Lakini mida yao ndo ishawadia, saa hazirudi nyuma zinasonga mbele