Naomba Mnishauri nilime zao gani

tuko pamoja mkuu tutachekiana kwa info zaidi
 
Pamoja Mr Varius..

Natamani sana nitembelee maeneo hayo kwaajili ya kupata taarifa zaidi, na ninaimani ntafanya hvo soon

saizi nipo nje kidogo Mbeya
 
Mkuu xplastaz nakushukuru sana...
Ningependa kufahamu hio 110,000/= ni bei ya Mbeya au Dsm...

Pili ningependa kufahamu huwa mna uza mpunga au mchele, kwamfano hio bei ni ya guniaa la mpunga au mchele?

Tatu naomba kufahamu ni mazao gani mengine yanayolimwa hapo Mbalali, na je kuna umwagiliaji wa uhakika katika mazao hayo mengine mbali na Mpunga
Nashukuru tena.
 
Nna ndoto kama zako, ntakuwa na mtaji wa millioni 4 niliwaza kulima mihogo mwezi wa 9 ili nivune mwezi wa tano kipindi cha mfungo panapo uzima, ntalima mihogo hekari 3 kwakuwa nna advantage ya kuwa na shamba sio la kukodi, pesa kiasi ntafanya ufugaji ili incase mambo yakiwa sawa mwaka ujao nnaamini ntakuwa na capital ya kutosha nifanye kilimo kwa kiwango kikubwa zaidi hasa mpunga na mihogo. Nna hofu ya kuingiza pesa yote sehemu moja kwa sasa cz mtaji ni wa manati aisee
 
Nakushauri pia pigia uzi wa kilimo cha mboga mboga hapo kwenye stick threads juu kabisa!! Utapa ujuzi pia!
 
Kuna mdau amekushauri Kulima mpunga ambapo naona ni ushauri mzuri. Uzuri wa mpunga hauna mahitaji mengi sana kama Mazao mengine. Ila sehemu utakayolima lazima iwe na maji ya uhakika. Swala la ndege inategemea na Eneo kwa mfano mie nimelima mambi nyuma ya igurusi msimu na tatizo la ndege sijalipata. Kwa kifupi hakuna utakachoamua kulima kitakuwa hakina changamoto, kila kitu kinachangamoto zake ni jinsi ya kujipanga kukabiliana nazo.
Ushauri wangu ukishaamua zao la kulima jaribu kulifanyia utafiti wake kwanza na usilewe na Yale mahesabu yetu juu juu ujione ushakuwa tajiri. Kuna changamoto nyingi ambapo usipojipanga utaamua. Ila ukifanya utafiti wako vizuri ukauliza na kwa watu waliolima jaribu kuanza na Eneo Dogo ili uweze kujifunza uzuri na changamoto za hicho kilimo. Mara nyingi msimu wa kwanza wa kilimo tunaita msimu wa kujifunza tu. Ili msimu wa pili uje ukiwa umeshajifunza vya kutosha.
Usikatishwe tamaa ndugu yangu inawezekana na changamoto kwenye Jambo lolote ni kawaida nikujipanga tu.
Ukipata wazo zao gani unataka kulima unaweza kuniambia kama nitakuwa na lolote la kukueleza nitakuambia Mimi napatikana Uyole.
 

Mkuu ulichokiongea hapo juu hasahasa kwny gharama za ekari moja ni kweli kabisa. Na kwenye la mbolea nadhani unalifahamu Hilo kama usipotumia mbolea ya SA kwa mashamba ya highland estates mavuno yanakuwa madogo mno sababu Kubwa ikiwa eneo hili limekuwa na chumvi sana na siku hadi siku inazidi kuongezekA ndio maana kuna kuwa na ulazima wa kutumia mbolea ya SA. Ila bado wanalima na kupata mavuno Yao. Kwny maelezo yako hapo umenikumbusha baadhi ya vitu kwenye hayo mashamba
 
Daah umeongea ukweli mtupu, ila nimecheka sana jinsi ulivyowasilisha.
 
[emoji120]
 
Kwa sasa ni 100000 na hii ni bei ya huku mbeya nilipo, binafsi sijawah kufanya biashara ya mchele huwa nauza mpunga tu na hiyo bei ni kwa gunia LA mpunga sio mchele, huku mbarali mbali na kilimo cha mpunga pia kwa miaka ya hivi karibuni kilimo cha mabustani ya vitunguu, nyanya, matikiti, mboga mboga kimeshamiri kwel kuna sehemu panaitwa igawa kuna mashamba makubwa ya vitunguu eneo LA Igomelo. Kwa upande huo sijajua changamoto zao maana sijawah kulima mazao hayo kwa eneo hilo ambalo kwa huku ndo maarufu kwa kilimo hicho.
 

kwanza kula senks kwa maneno ya busara {huu ndio tunauita u-great think sio kushauliana kulima bangi hapa} nimependa flow yako iko so nice.. pia unapenda ushirikiano thats very nice.. watu kama nyie na wengine wote walio toa +ve comments MUNGU huwa anawabariki kwa style ya mafanikio kwenye kazi za mikono yenu, nazan mtoa uzi atapata cha kufanya juu ya hili
 
Wote tunahangaika, kikubwa kupeana support kila mmoja kwa nafasi yake na uwezo wake. Tupo pamoja mkuu, big up
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…