Kwanza nakukaribisha Jukwaani, Karibu the Home of GT.
Pili, hongera kwa matokeo yako. Lakini kwa matokeo hayo, japokuwa umefanya vizuri Kupata nafasi ya kusoma MD katika Chuo cha Afya Muhimbili, inakuwa ngumu kidogo. Kuna competition kubwa sana. Biology imekuangusha kidogo lakini jaribu waweza kufanikiwa.
UDSM, medicine ilikuwepo. Lakini Mh Rais alitoa Ushauri ifutwe na kwa mantiki hiyo sidhani kama Mwaka huu watadahili. Hivyo hakuna. SUA haijawahi kuwa na MD. Labda Udaktari wa Mifugo lakini si wa binadamu. Kwa hiyo SUA pia hakuna.
Pindi wwatakapoanza kupokea Maombi ya Udahili kupitia chuoni moja kwa moja, nakushauri fika mapema au fanya utaratibu wote utakaotolewa na Chuo husika uweze kuangaliana uwezekano wa Kudahiliwa.
Turudi kwa Mdogo wako;
Kozi za afya ikiwa ni pamoja na Unesi, Clinical Officers, Labaratory technicians pamoja na nyinginezo huombewa katika tovuti ya NACTE,
www.nacte.go.tz
Hivyo mdogo wako, atapaswa kufuata taratibu zote na aombe chuo husika na kama atakuwa na matokeo ya kuridhisha atapangiwa Chuo cha Muhimbili katika kozi yake.
Nakutakia kila la kheri.