Habari za mchana wanajamii,
NAOMBENI MBINU ZA KUISHI NA MUME BAHILI/MCHOYO. mwanaume ni mchoyo jamani, vitu viikisha ndani atajikausha utafikiri sio yeye ndo baba wafamilia. umeme unakatika atauchuna na mtalala gizani, asubuhi ataondoka bila kuacha hata mia sijui anawaza mtakula nini, kwakuwa nina mtoto mdogo na wadada wa kazi inabidi niwaachachie pesa za matumizi, gari akiriharibu hatengenezi ng'o na litaendeshwa hivyo hivyo mpka utakavyoamua kulipeleka gereji mwenyewe.nimechoka jamani basi ikokea katoa hela utakuta kaweka 100000 kabatini na hakwambii kama ni pesa ya matumizi. akishatoa hiyo atajikausha hata miezi mmine inaweza pita bila kutoa kitu. na bado ataendelea kukuomba hela,mara naomba hela nikaweke mafuta kwenye gari, mara naomba hela ya sadaka ili mradi ile aliotoa mpaka iishe. Basi nikafunguabiashara sehemu, akaidakia yeye akaanza kuisimamia, sijawahi ona hata mia kutoka kwenye ile biashara, kodi ya pango ikaisha, hela hata mia, ikabidi nilipie tena kodi, bado sioni kitu yaani kama hakuna biashara inaendelea,ukimuuliza anakuwa mkaliii.basi nimeamua kutolipa tena kodi ya pango ikiisha, na TRA Silipi. nimemsema sana lakini naona habadiliki. nimfanyeje mwanaume wa hivi khaaaa