Naomba mbinu za kuishi na mume bahili

marrykate

JF-Expert Member
Mar 4, 2012
733
442
Habari za mchana wanajamii,

Naombeni mbinu za kuishi na mume bahili/mchoyo.

Mwanaume ni mchoyo jamani, vitu viikisha ndani atajikausha utafikiri sio yeye ndo baba wafamilia. Umeme unakatika atauchuna na mtalala gizani, asubuhi ataondoka bila kuacha hata mia sijui anawaza mtakula nini, kwakuwa nina mtoto mdogo na wadada wa kazi inabidi niwaachachie pesa za matumizi, gari akiriharibu hatengenezi ng'o na litaendeshwa hivyo hivyo mpaka utakavyoamua kulipeleka gereji mwenyewe.

Nimechoka jamani basi ikokea katoa hela utakuta kaweka 100,000 kabatini na hakwambii kama ni pesa ya matumizi.

Akishatoa hiyo atajikausha hata miezi minne inaweza pita bila kutoa kitu na bado ataendelea kukuomba hela,mara naomba hela nikaweke mafuta kwenye gari, mara naomba hela ya sadaka ili mradi ile aliotoa mpaka iishe.

Basi nikafungua biashara sehemu, akaidakia yeye akaanza kuisimamia, sijawahi ona hata mia kutoka kwenye ile biashara, kodi ya pango ikaisha, hela hata mia, ikabidi nilipie tena kodi, bado sioni kitu yaani kama hakuna biashara inaendelea,ukimuuliza anakuwa mkali

Basi nimeamua kutolipa tena kodi ya pango ikiisha, na TRA Silipi. Nimemsema sana lakini naona habadiliki.

Nimfanyeje mwanaume wa hivi khaaaa
 
Habari za mchana wanajamii,
NAOMBENI MBINU ZA KUISHI NA MUME BAHILI/MCHOYO. mwanaume ni mchoyo jamani, vitu viikisha ndani atajikausha utafikiri sio yeye ndo baba wafamilia. umeme unakatika atauchuna na mtalala gizani, asubuhi ataondoka bila kuacha hata mia sijui anawaza mtakula nini, kwakuwa nina mtoto mdogo na wadada wa kazi inabidi niwaachachie pesa za matumizi, gari akiriharibu hatengenezi ng'o na litaendeshwa hivyo hivyo mpka utakavyoamua kulipeleka gereji mwenyewe.nimechoka jamani basi ikokea katoa hela utakuta kaweka 100000 kabatini na hakwambii kama ni pesa ya matumizi. akishatoa hiyo atajikausha hata miezi mmine inaweza pita bila kutoa kitu. na bado ataendelea kukuomba hela,mara naomba hela nikaweke mafuta kwenye gari, mara naomba hela ya sadaka ili mradi ile aliotoa mpaka iishe. Basi nikafunguabiashara sehemu, akaidakia yeye akaanza kuisimamia, sijawahi ona hata mia kutoka kwenye ile biashara, kodi ya pango ikaisha, hela hata mia, ikabidi nilipie tena kodi, bado sioni kitu yaani kama hakuna biashara inaendelea,ukimuuliza anakuwa mkaliii.basi nimeamua kutolipa tena kodi ya pango ikiisha, na TRA Silipi. nimemsema sana lakini naona habadiliki. nimfanyeje mwanaume wa hivi khaaaa
Sasa wewe umeoa SERENGETI BOY halafu unakuja kuomba ushauri humu?,mtu mpaka anaendesha gari lako,hela ya mafuta akuombe wewe halafu bado hujajua kua ni mume au serengeti boy?,SEMA UMEMCHOKA mpige chini tafuta real man
 
Kwan mlikutana kwenye ndoa tu s mlianza uchumba ukutambua aya
kwakweli wakati wa uchumba alikuwa na hali ngumu kimaisha so alikuwa hatoi kitu, mi nikachukulia poa tu, nikahisi vile hana ndo maana hatoi, ila kwa sasa pesa anayo
 
Aliyekutuma ujitongozeshe kwa mwanaume kisa ana sura nzuri ndo huyo huyo akakupe ushauri...

Fanya kazi pata hela,mnunulie nguo kauze nae sura.


Kama sio hivyo basi humpi ngono nzuri hivyo mwanaume hapotezi mda kugharamikia mwanamke ambaye hata waki sex nae Ni kwasababu anataka ku release tension, no intimacy.
 
Back
Top Bottom