Naomba Mamlaka ya Maji Safi na Taka Mbeya ifutwe, wanalipwa mishahara bila kazi

CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,789
1,782
Mamlaka ya maji Mbeya wafanyakazi wake hawastahili kulipwa mishahara kwa sababu hakuna wanachokifanya na hawapo pale kutoa huduma ya maji kwa wananchi. Wapo kama TRA tu yaani kukusanya pesa basi.

Ni miezi 4 sasa eneo la Uyole 90% ya bomba hazitoi maji. Wakilalamikiwa hawatoi msaada wowote. Kibaya zaidi bili za maji zinakuja kila mwezi, yaani hata hewa inayokoroma kwenye bomba inatolewa bili. Usipolipa wanachimba mkwara eti utapigwa faini.

Kipindi fulani walifanya usanii eti wakatuma wataalam kuzunguka nyumba kwa nyumba kubaini ni nyumba zipi hazina maji. Walipoondoka ikawa ndio imetoka hakuna mrejesho wala nini.

Nyumba chache zinazotoa maji wanaogopa kusaidia wasio na maji maana wakijua unauza maji bili utakayoletewa utajuta.

Tunatumia maji ya madumu ambapo dumu moja ni shilingi 300. Kama mahitaji yako ni madumu 10 kwa siku hiyo ni shilingi 3000 kila siku. Kwa mwezi ni sh 90,000! Kwa uchumi upi? Hapo bado kujaletewa bili ya sh 30000 ili ulipie hewa! Maji haya yanachotwa kwenye visima navyo nasikia wameanza kuvifuatilia! Yaani hawashughulikii tatizo wanafuatilia watu wanasaidia kutatua tatizo.

Yaani hawa waheshimiwa hawajawahi kuja kueleza tatizo ni nini na wanafanya nini kutatua au wana mipango gani! Wamekaa tu ofisini kama TRA wanasubiri hela na kulipwa mishahara mwisho wa mwezi.

Naomba Mamlaka zilizo juu yao wawasimamishie mishahara mpaka waweke wazi umuhimu wa kuwepo kwenye pay roll.

Mbona TANESCO kukiwa na tatizo wanatoa taarifa na wanalishughukia haraka?
Hii mamlaka ya maji Mbeya natamani ifutwe kabisa sijui waliisomea kufungua bomba zinazotoa maji tu hawakusomea kutatua changamoto za maji?
 
Poleni, Mimi niwapongeze mamlaka ya maji safi na maji taka Kahama(KUWASA), wanajitahidi sana, TANESCO wanakwama sana.
 
Njoo pm nikupe mchongo wa uchimbaji kisima
 
Hawa jamaa ni hovyo hatari.
Mimi mwenyewe nipo kalobe huku niliibiwa mita ya maji toka mwezi wa 4 mwaka huu lkn cha kushangaza nilikuwa natumiwa bili kila mwezi mpaka mwezi wa 9 na wanaandika nimetumia unit kadhaa kila mwezi.
Niliporudi toka safari nikawanyokea wanachekacheka tu.
Nikawaambia futeni hiyo bili wakasema sheria hairuhusu.
Hovyo kabisa hawa
 
Yaani wanatia hasira sana
 
Back
Top Bottom