Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Jijini Mwanza (MWAUWASA) mnatakiwa kujitafakari

Torra Siabba

Senior Member
Jul 24, 2016
105
102
Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka jijini Mwanza (MWAUWASA) mnatakiwa kujitafakari kutokana na utendaji kazi wenu mbovu ambao mwisho wa siku kama msipokemewa yatakuwa mazoea sasa.

Hivi sasa ni wiki ya pili Barabara ya Posta jirani na Benki ya Kilimo Katikati ya jiji la Mwanza kuna Chemba ya Maji taka limepasuka na bahati mbaya ni kwamba maji hayo machafu yanatiririka kukatiza barabara mpaka unajiuliza hivi hawa watu wa mamlaka ya maji safi na maji taka wako wapi?

Kama bomba la majitaka liko katikati ya jiji linapasuka na hawachukui hatua za haraka je Likipasuka Buswelu sindio linamaliza Mwaka kabisa? ifike mahali mtimize majukumu yenu bila kukumbushwa.

20230605_144030.jpg
 
Back
Top Bottom