Mkimuyangu
JF-Expert Member
- Oct 5, 2022
- 1,054
- 1,947
Naomba kuwauliza kina dada humu ndani, kuna binti mmoja nilitaka kumuoa lakini akanikatalia kwa kigezo hawezi kuolewa na mimi kwa sababu ni bosi wake.
Kiukweli huyu binti nilitafutiwa na mtu kwa ajili ya kuja kunisaidia kuuza duka langu, lakini siku zilivyokuwa zinakwenda kutokana na kuikubali tabia yake nikaanza kupanga kumuoa.
Lakini alinikatalia na kuniambia hawezi kuolewa na mimi kwani ni bosi wake, baadaye akaja kuolewa na mtu mwingine na akaacha kazi. Sasa kinachonifanya kuja kuuliza, muda mwingi amekuwa akiniambia vitu vyake vya siri, anaishia kuniambia, unayejua wewe na mume wangu tu, usimwambie mtu.
Mfano alikuwa anaumwa akanipigia simu ameenda hospital kakutwa mja mzito lakini nisimwambie mtu, najua mimi tu na mme wake, kama wanawake hii inaleta picha gani? Na bado muda mwingi ananipiga mizinga, akija dukani lazima aombe vitu, ingawa huwa nampa kila anachotaka, lakini nimeanza kujistukia labda ananichukulia bwege?