Naomba kuuliza bei ya hii pikipiki

click hio ni ndege.kwanza ina rejeta ina spid boxa ihaifikii.zipo mpka za milion 8
Upo sahihi kinachofanya bei ya Honda Click kuwa juu ni teknolojia iliyowekwa.

Hizo pikipiki zina rejeta Kwa ajili ya kupooza injini (liquid cooling) wakati pikipiki ndogo nyingi zinatumia mfumo wa hewa (air cooled).

Pia kwenye zina mfumo wa fuel injection wakati wengine bado wanatumia carburetor.
Hizi pikipiki hazina nyororo ni mwendo wa mkanda (driving belt), sasa kuna matoleo ambayo inakuwa na keyless na security alarm system.


Wachina wanazo Shineray kama hii Click ukiendesha utaona tofauti na mifumo waliyoweka.Mhindi anazo zinaitwa Mahindra Gusto, wanaendesha wenyewe raia wanaziangalia Tu hapa Bongo.
 
Kuna uzi humu jamaa anaziuza toka zanzibar, aliweka bei yake milioni 3.5

Zingatia, sijawahi fanya nae biashara, sijui kama ni muaminifu ama tapeli.
 
Back
Top Bottom