Kwa bei hii ya Honda niichukue kwa ajili ya biashara ya Boda?

3 Angels message

JF-Expert Member
Aug 3, 2017
4,890
13,633
Wakuu habarini za wakati huu? Binafsi niko poa kabisa namshukuru Mungu

Siku ya leo nilipata tena nafasi kutembelea maonesho ya sabasaba na lengo kuu ilikuwa kwenda kununua miche ya matunda banda la maliasili na utalii.

Wakati napita nikasikia bwana mmoja akinadi kuwa anauza pikipiki kwa bei ya hasara nikavutiwa naye maana nina mpango wa kuvuta pikipiki kwa ajili ya biashara ikabidi nisogee kuona ni pikipiki aina gani kufika nikakuta ni pikipiki aina ya Honda bei zake 1.7m hii ni ya kupiga kiki na nyingine ni 2.1 m hii siyo ya kupiga kiki

Hii ikaniweka njia panda maana siku ya nyuma nilipita kwenye banda lingine linalouza pikipiki aina ya boxer bei ilikuwa 2.6 m kwa 2.7

Swali langu hizi honda ziko vizuri nichukue vipi spare zake zinapatikana pia maana nimeona bei zake ni nafuu kuliko boxer
 
Wakuu zipo kama hii honda zenyewe
Screenshot_20230714-105847.jpg
 
Back
Top Bottom