Naomba kutajiwa faida za dini

Naomba kutajiwa faida za dini

Sipajui mkuu, ila dini inatufundisha ndipo tutaenda kuishi daima na milele baada ya ufufuo wa ki roho kutokana na kifo cha hapa duniani kama tutafata amri zilizoshushwa na Muumba.
dini Ni fumbo kubwa sana bila shaka
 
Mpaka sasa nafikisha miaka 43,nimeijua moja tu,nayo ni kusaidia kwenye elimu, nje ya hapo sijaona
Hapa nazungumzia UKRISTO NA UISLAMU.
Faida za Dini
1- unapata kujua chanzo Cha mwanadamu pia historia, Dini imeelezea Ila sayansi inakuja kuprove
2- ukiwa mfuasi wa Dini Kuna ahadi ya malipo baada kufa
.
.
Etc.
 
Mkuu Iran,Israel,Iraq,Syria amani hakuna
Upande wa maadili angalia wadangaji,washerati, wezi,Mafisadi,WANASIASA wao ni zero
Hapo sikutaja au kushadidia Taifa, nchi au kundi!!
Nimetoa faida za Mtu (binafsi) mwenendo wa binaadamu aliye kamilika...
 
Faida zake:-.
Kuishi kwa Amani
Kuishi kwa maadili
Kuishi na binadamu wenzio (ndg. Jirani, wenza,nk nk) kea heshima na muamala, desturi.
Kutii amri za Muumba na kuomba msamaha unapohisi au kukosea..
Kutunza familia yako bila kubaka wanao!!! (Niwieradhi)
Kujenga matumaini ya ahera (maisha baada KIFO chako)

Karibu nikutsmbulishe Mwenyezi Mungu na sifa zake.
Mkuu Iran,Israel,Iraq,Syria amani hakuna
Upande wa maadili angalia wadangaji,washerati, wezi,Mafisadi,WANASIASA wao ni zero
 
Mpaka sasa nafikisha miaka 43,nimeijua moja tu,nayo ni kusaidia kwenye elimu, nje ya hapo sijaona
Hapa nazungumzia UKRISTO NA UISLAMU.
Dini zinafaida zaidi ya hiyo uliyoitaja wewe, husasani kwa mtu mwenye Imani katika dini yake. Iko hivi binadamu ni mnyama Kama wengine lakini mwenye utambuzi wa level ya juu kuliko hao wengine katika kumudu mazingira yake. Ili binadamu awe na utu, dini huchangi pakubwa. Dini kwa mwenye kuamini ni kiunganishi au daraja la kuamini uwepo wa supernatural being, ambaye ni mwanzo na mwisho wa kuamua uhai wako. Huyo ndie tunamwita Mungu. Binadamu asiye amini uwepo wa supernatural being (God),huyo ni zaidi ya wanyama hatari unaowajua wewe. Hana utu ndani yake bali element za uovu. Sasa faida yake dini ni kuunganisha na supernatural being, ambaye yeye huamua hatima yako. Ukiamini ktk dini, tabia yako unakuwa regulated kuenenda kwenye misingi ya kiutu, kwa hofu ya kumkosea huyo supernatural being. Ukiwa muonga wa matendo yanayo muudhi (dhambi), unaingia sehemu nzuri aliyokuandalia after your life expires on Earth.
Dini kwa anaye amini inapatanisha penye chuki. Dini inaponya mtu aliyesongwa na shida za dunia hii Kama vile, kufirisika, kutokuwa na ajira, kuachwa na mpenzi, kufiwa, kufungwa bila kosa na mengineo. Nimesema ukiamini katika dini yako utaona jinsi utakavyoponywa.
 
Dini ina umuhimu kwa Waislamu ila kwa upande wa wafuasi wa Yesu ( Wakristo) dini haina maana yoyote.Katika Biblia hakuna sehemu yoyote ambayo Yesu alisema alileta Ukristo.Hata agano la kale halijataja Ukristo.

Isipokuwa mataifa(Walimwengu) ndio waliwaita wafuasi wa Yesu Wakristo,kwa sababu ya kuwa na tabia na matendo km ya Yesu. Mtu anaeng'ang'ania dini yuko tayari kuua mtu mwingine ili kutetea dini yake,kitu ambacho ni zaidi ya ujinga.
 
Ni mada ndefu sana ...naomba nikuulize unataka ufahamu au unataka kukejeli ?
 
Utaratibu uliowekwa ili kuwafanya watu wawe wastaarabu; ingawa wengine wametumia kama sehemu ya ajira...ndio maana sadaka na michango haiishi; swali la kujiuliza,wao walishakuchangia kiasi gani pale ulipokuwa na shida?
 
Dini ina umuhimu kwa Waislamu ila kwa upande wa wafuasi wa Yesu ( Wakristo) dini haina maana yoyote.Katika Biblia hakuna sehemu yoyote ambayo Yesu alisema alileta Ukristo.Hata agano la kale halijataja Ukristo.

Isipokuwa mataifa(Walimwengu) ndio waliwaita wafuasi wa Yesu Wakristo,kwa sababu ya kuwa na tabia na matendo km ya Yesu. Mtu anaeng'ang'ania dini yuko tayari kuua mtu mwingine ili kutetea dini yake,kitu ambacho ni zaidi ya ujinga.
Daah! hiki ulichokiandika hatari sana
 
Binadamu kama walivyo wanyama wanaofanana nae huwinda ama huishi kwa makundi (bands) hizi bands zinatofautiana kulingana na aina ya mnyama ( sokwe,ngedere,nyani) kwa binadamu idadi ina range 150 -500 sasa tofati na wanyama wengine binadamu anauwezo wa kufikiria vitu visivyokuwepo , uwezo huu ukaanza kutumiwa ili kuunganisha watu zaidi ya idadi ile ambayo ina limitation hapa ndio Dini zikaanza kuzaliwa...hivyo basi IMANI (dini,utaifa) ni muhimu kuunganisha watu tofauti na hapo tusingefika hapa tulipo hata mataifa kama North Korea yanaojinasibu hayana dini unakuta technically wanaabudu viongozi wao kama miungu ...hizo Dini ni moja ya mifano hai wakristo duniani kote wanaunganishwa hivyohivyo waislam mwezi wa ramadhani wanaungana dunia nzima ...Kiimani siwezi kuelezea kwa sababu utaniuliza ushahidi ... kiafya Dini inawapa ahueni na matumaini watu na pia inasaidia ku-shape mienendo ya watu ...
 
Dini ni msaada kwa watawala na viongozi kuwatawala kijamii,kisiasa na kiuchumi watu walio chini yao!!!Wakatoliki hiyo unaiona wazi kabisa tena kama una akili timamu hata kwa waislam ivo ivo!!Masuala ya uzima wa milele na peponi kama zawadi kwa wafia dini hayana LOGIC !!JIULIZE :-Inakuaje mtu aishi miaka labda 60 afe halafu ahukumiwe kwa miaka isiyoisha yaani milele anachomwa moto kwann asihukumiwe kwa miaka 60????
 
Back
Top Bottom