Protein supplement sio mwisho wa kila kitu, formula ya kuongezeka mwili ni simiple tu, calories unazoingiza mwilini zizidi calories unazoburn. So piga hesabu ujue mwili wako unahitaji calories ngapi alafu kula kama 300-500 calories zaidi ya hiyo utaanza kuongezeka uzito.
Sasa ili usiongezeke kitambi hapo ndo inakuja inabidi uongeze calories nzuri, protein ni sawa, fat pia si mbaya, carbohydrate kidogo usisahau muhimu kwa sababu ya energy la si hivyo chumba utashindwa kunyanyua.
Protein supplement karibia zote ni sawa tu, angalia yenye protein content nyingi na bcmaa, angalia ladha unayopenda kuna chocolate, vanilla, coffee e.t.c then tumia. Ila kula vizuri, supplement ni extra tu usigeuze iwe meal yako. Kama upo ka wabongo wengine unakula ugali sana punguza, ongeza chicken breasts, maharage, wali kidogo, ugali potezea kabisa au kula kidogo sana.
Fata hayo baada ya kama mwaka hivi utakua na mwili safi, miaka mitatu huo uliouweka hapo utauona wa kawaida sana.