Naomba kujuzwa wakuu kuhusu mitihani ya CPA,CPB na PSPTB

beneli

Member
May 1, 2013
86
7
Habarini za jioni wakuu, mabibi na mabwana, natumai wote mu wazima baada ya kushereheka na sikukuu ya pasaka.
lengo kuu lilonisukuma kuandika swala hili ni ujuzi wa mambo ambao wanajukwaa mmebarikiwa kuwa nao hasa katika kutoa ushauri wa kina katika maswala ya elimu.

Wakuu mimi ni mwanafunzi ninaekaribia kumaliza shahada yangu ya uongozi wa biashara yaani BBA General ambayo hijaegemea upande wowote, natamani kupata nafasi ya kufanya mitihani ya umahiri ama professional exams kama CPA au CPB ama ya bodi ya manunuzi PSPTB.

Wakuu naomba mtu mwenye uelewa mzuri hasa katika CPA na PSPTB , Je mtu kama mimi anaanza level gani ?
Ama ipi njia bora zaidi ya kufuata niweze kufikia lengo la kuwa na professional qualification mapema ?
Naomba msaada wenu wakuu.
 
Kwa CPA(T) utaanzia Foundation stage masomo 05 na watakupa exemption endapo kuna masomo katika ngazi hiyo uliyasoma chuo, baada ya hapo utasoma Intermediate stage masomo 06 na hatimae Final stage msomo 04, Gharama kwa mlolongo wote kwa centre kama Arusha, Dar es Salaam na Mwanza kwa kuanzia uwe kama na milioni moja unusu hivi kama si mwenyeji wa maeneo hayo na kama ni mweneyeji zinaweza zikashuka, na hapo nimeweka gharama za msosi, usajili,pepa,review tu kwa foundation stage tena kama utapata exemption, Nauli,steshenari,na malazi unajiongeza mwenyewe.
 
Ingia kwenye website za hizo board husika utapata maelezo yote.! Kwa CPB ingia kwenye website ya Tanzania Institute of Bankers kila kitu kipo wazi
 
Back
Top Bottom