Naomba kujuzwa utaratibu wa uhamisho wa shule kwa mwanangu

Sheffer95

Senior Member
Mar 16, 2020
197
460
Habari za muda huu Wana JF. Nilikuwa naulizia utaratibu kwa mtu anayefahamu kuhusu kumuhamisha mtoto wa secondary form one kutoka shule moja kwenda nyingine na ni mkoa tofauti.

Namuhamisha kutoka iringa kwenda Dodoma ambao nimehamia.

Natanguliza shukran zangu🙏
 
Kwanza kabisa itakubidi kutafuta shule ya kumuhamishia mwanao ww mwenyewe,kisha utaenda kumuomba mkuu wa shule unayotaka kumuhamisha mwanao,...ni lazima mkuu huyo wa shule akubali kumpokea ndio uendelee na process nyingine,,...hapo kwenye kuongea na mkuu wa shule unapomuhamishia ndio pagumu sana,na hapo ndio wakuu wa shule nzuri za serikali wanapopiga hela,,na by the way ukishamalizana na mkuu huyo wa shule anayohamia bac mchezo umeisha maana hapo ndio pagumu,huku kwingine utakua unapita na li barua lako kutafuta saini tu.kama mkuu anazingua muoneshe harufu ya hela tu,,kuhusu kiasi cha pesa utakayompa inategemea na ubora wa elimu shuleni hapo(hii ni rushwa Ili Ili mwanao apokelewe) japo shule nyingine unaweza kukubaliwa free bila chochote,kumbuka kuwa hakuna cha afisa elimu wala nani anaweza kukusaidia kumwingiza mwanao hapo shuleni bila mkuu wa shule hio kukubali kuwa anayo nafasi ya kumpokea,anaweza kusema kuwa nafasi zimejaa na hawez kumpokea na hakuna wa kumlazimisha ila tu walimu wakuu wengi wanawaogopa mabosi wao(maafisa elimu),hivyo km kuna mkubwa anaeweza kukusaidia bac waweza kumtumia huyo.ukikubaliwa utaandika barua yenye sababu za maana za kwa nini unamuhamisha mwanao shule,unaeza sema kuwa na wewe km mzazi/mlezi unahama,barua hiyo unaiandika kwa afisa elimu mkoa kama anahama nje ya mkoa au afisa elimu wilaya kama anahamia shule ya wilaya hiyo hiyo,kisha utaielekeza I mean itapita kwa mkuu wa shule alopangiwa (anaposomea)-huyu ataipitisha kwa kukubali kumhamisha(hapa hapanaga ugumu),kisha utaielekeza tena kwa mkuu wa shule anayohamia---kule ulipoenda kuomba nafasi ya kumhalishia(hapa ndio mziki)--nae huyu atasain na kukubali kumpokea mwanafunzi,,kisha utaielekeza barua yako kwa afisa elimu wilaya,then mkoa anaotoka na mwisho ni kwa afisa elimu wilaya na mkoa anapoend.....hapo mchezo umeisha mkuu,,ni ka process flan hv kareefu na kanakero sana maana watia sain ni wengi lkn km una connection unamaliza kila kitu chap chap.kila LA heri mkuu,mpekeke mtt akasome shule nzur.
NB-walimu wakuu wengi wanapenda kuangalia mwanafunzi wanayempokea anakuwa na uwezo mzuri darasani,,kama ni wa form one bac watataka kuona wastan wa matokea yake ya mtihani wa drs LA saba na wengi wanataka wtt wenye wastan wa A au B pekee wakihofia kuchukua vilaza,na km mwanafunzi yupo form two na kuendelea watataka matokea yake ya shule kwa muhula ulopita,wakikuta ma F na D ya kutosha my friend utasota sana,angalau mtt akiwa vzr kiçhwani wanampokea fasta maana wanajua hiyo ni division 1 au two

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom