Naomba kujuzwa ubora wa Probox na Toyota Wish

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
5,018
2,000
Wakuu naomba mtaalam wa magari anipe ufafanuzi wa ubora wa hizi gari nilizotaja hapo juu! Dadavua kadri unavyofahamu!
 
Nov 21, 2017
45
125
Wakuu naomba mtaalam wa magari anipe ufafanuzi wa ubora wa hizi gari nilizotaja hapo juu! Dadavua kadri unavyofahamu!
Probox ni ngumu kuliko Wish. Nimeziona sehemu mbalimbali hasa mkoani Kigoma zikiwa ndio gari za kubebea mizigo kwenda magulioni,Pia nchini DRC ndio gari za mizigo na taxi. Zinabeba mizigo hatari na zinavumilia.Na Engine yake ni ndogo ukilinganisha na wish. Wish IPO kwa luxury zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
5,018
2,000
Probox ni ngumu kuliko Wish.Nimeziona sehemu mbalimbali hasa mkoani Kigoma zikiwa ndio gari za kubebea mizigo kwenda magulioni,Pia nchini DRC ndio gari za mizigo na taxi.Zinabeba mizigo hatari na zinavumilia.Na Engine yake ni ndogo ukilinganisha na wish.Wish IPO kwa luxury zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo umesema kweli Dada Eliza, nimekaa Kibondo muda mrefu mchomoko za pale zote ni Probox mpaka nikawa nashangaa mwenyewe kwa nini? Pale Nyakanazi napo asilimia kubwa ni Probox! Kuna siri hapo! Luna mwingine akaniambia mafuta huwa vinanusa tu!
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
5,018
2,000
Nunua Probox/Succeed. Ni ngumu sana. Kigoma, Geita, Kagera na baadhi ya maeneo ya Shinyanga ndio gari za kuaminika za abiria.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kweli, nitakatumia kwenda kazini kati ya Mwanza na SHY. Huwa naenda J3 na kurudi Ijumaa, sasa ninaporudi naweka mzigo wa dukani nafikri unavyoshauri katanifaa sana kubeba mzigo!
 

Prodigy Oligarchy

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
260
250
Wakuu naomba mtaalam wa magari anipe ufafanuzi wa ubora wa hizi gari nilizotaja hapo juu! Dadavua kadri unavyofahamu!
Ni kitu ambacho wala hakina haja ya kufafanua sana.

Probox, ni wagon iliyobuniwa na kutengenezwa maalum kwaajili ya biashara ya usafirishaji haswa mizigo -mizigo.

Ni gari imara na ngumu sana kiukweli, na ambazo zinahimili uzito pamoja na ubovu wa barabara .. na ndio maana hata ambao wapo vijijini n.k wanazitumia sana kama daladala na gari za kubebea mizigo.

Zenye 1,490 cc (1,500cc) hua zinatembea 15.8km/L
Na zenye 1,290cc (1,300) hua zinatembea 16.0km/L
 
Top Bottom