Hakika Haya maneno yananisumbua kuyaelezea kwa tafsiri sahihi.
Naishia kusema tu mtu ni binadamu na binadamu ni Mtu.
Karibuni wataharamu wa lugha. Munisaidie Kunipa tofauti Ya haya Maneno.
Asante
Japo watu wametoa ufafanuzi ngoja na mimi nitoe kidogo.
Watu ni jamii yote ya viumbe wa makundi fulani wa wanyama wanaihusiana kigenetic na wanaoweza kuzaliana wakikutana kimapenzi, wataalamu wa (mambo ya kale) waliweza kuweka makundi hayo ya watu na kuyapa majina kulingana na maeneo walipotoka, mfano kuna Homohabilis, Homo erectus, zinjanthropus nk, hadi leo akatokea Homosapiens ambao ndio sisi.
Hapo sasa utaona watu wamepitia hatua ndefu mbalimbali mbali hadi hii leo.
Binadamu ni nani???--- ubinadamu ni sifa anayokuwa nayo mtu, kifupi mtu akistaarabika huyo ataitwa binadamu, kifupi ni kwamba mtu wa kwanza kuleta ustaarabu duniani ni Adam (Nabii Adam as), huyu aliletwa/alitumwa na Mungu kwa watu wake kuja kuwafundisha maadili mema, yeye alikuwa mtu wa KWANZA kuwa mstaarabu (civilized) bali hakuwa mtu wa kwanza kuumbwa kama watu wengi wanavyoamini kimakosa.
Kwakuwa Adamu ndiye mtu wa kwanza katika hili kundi letu la Homosapiens kuwa na maadili na ustaarabu ndipo sisi watu waleo tukiwa na maadili mema na ustaarabu pia tunaitwa Wanaadamu (wana wa Adamu) au watoto wa adamu tunaitwa hivyo kwa heshima ya huyo Adamu tu.
Hivyo ubinadamu wa mtu ni sifa njema za kimaadili alizokuwanazo mtu yeyote na ndipo mtu huyo huitwa Binadamu.