Naomba kujuzwa ripoti ya ESCROW itasomwa saa ngapi

Naomba kujuzwa ripoti ya ESCROW itasomwa saa ngapi

reandle

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
11,166
Reaction score
8,152
Hivi sasa tunahesabu saa kuelekea 26/11/2014 siku ambayo tunataraji ripoti ya CAG kusomwa bungeni! Hapahitaji shahada kufahamu kwamba hii itakuwa ni ripoti mbaya kabisa kupata kutokea katika ukanda huu wa Afrika. Hii ni ripoti ambayo Mtanzania hatakiwi kuikosa wakati inasomwa, iwe kupitia TV, radio, internet or else!

Pamoja na yote hayo, wewe unaweza ukatamani kuifuitilia live hiyo ripoti lakini TANESCO wakakutamani zaidi usiifuatilie! Hii ripoti inawa-implicate hadi watu wa TANESCO kwahiyo hujuma may be expected! Wala tusishangae baadhi ya maeneo ya nchi yakiingia gizani kuanzia kesho ili isionekane TANESCO wamekata umeme ili watu wasifuatilie bunge... hivyo basi, busara ya kipumbavu kwao itakuwa ni kukata umeme saa kadhaa or probably a day or two kabla ya tukio lenyewe! Mimi si kama Yericko Nyerere kwamba nasema TANESCO watakata umeme ninachosema ni kwamba wanaweza kuhujumu!

Wale wanaoshinda nyumbani na hata wasioshinda nyumbani mnatakiwa kujiandaa dhidi ya hujuma zinazoweza kutokea ili kuwanyima haki yenu ya kupata habari! Siku hizi simu nyingi zina redio... je, una earphone? Kama huna fanya hima hima kununua kwavile the chance ya kuwepo umeme ni 50%,50%. Je, betri ya simu inahimiri kukaa muda mrefu? Kama hapana, siku hiyo jihdhari matumizi yanayotumia sana betri! Heri unaebaki home unaweza ku-opt kununua betri kwenye radio ingawaje wengine radio zetu hata hiyo sehemu ya kuweka betri hakuna!!!

Don't worry ewe unaeenda kazini! Mjini kati hiyo jumatano itakuwa full heka heka... hakuna bosi atakayekuwa na ubavu wa kuzuia wafanyakazi wake wasifuatilie kinachoendelea Dom... kwanza hata bosi mwenyewe nae atakuwa anafuatilia! Hata wale mnaofanya kazi ambazo moja kwa moja mnakutana na wateja kwenye halls (banks, tel companies etc)... msiwe na wasi wasi; na wateja wenyewe hiyo siku watakuwa busy na watakuja in your halls na earphone zao masikioni.

Ni muhimu ukiifuatilia hii ripoti mwenyewe ili hata utakapojiingiza kwenye mijadala uwe unafahamu unajadili nini... leo hii hapa tukisema tujadiliane scandal ya Richmond ni wachache sana wanaoweza kujadili according to report... wengi tutajadili kwa rejea ya maneno ya kusikia!

Huo ni ushauri tu, ukitaka uchukue na kama vipi upotezee!
 
Jambo la maana... Ni siku ya watanganyika kujua mbichi na mbivu... Na kuwajua matumbili ni wapi?? Mimi binafsi nimeshachoka na mwendo wa sirikali inayotufanya wote hatuna akili. ENOUGH IS ENOUGH...... #bring back our money
 
Ahsante mkuu
Wengine hatukufikiria uwezekano wa hiyo hujuma
Tanzania ni zaidi ya uijuavyo ndugu yangu!! Hata Jesus ambae alidhani ni issue sana kwa ngamia kupenya kwenye tundu ya sindano, angerudi TZ leo hii angetoa reference nyingine coz' kwa Tanzania ngamia ana uwezo wa kupita kwenye tundu ya sindano sawa na sisimizi tu!!
 
Mkuu tumekusikia. Hiyo tar 26 Nov kila goti litapigwa. Nchi na dunia itazizima na akili, masikio ona macho ya wapenda TZ vitaelekezwa mjengoni... pamoja sana mkuu
 
Tunaisubiri hiyo ripoti kama mechi ya elcasico
 
Ushauri mwafaka.
Tuwaeleze pia ambao tunadhani hawapo JF.
Pia mkuu unaweza kuusambaza kupitia mitandao mingine kama Fb n.k
 
Wadau taarifa nimepata kuwa ripoti ya ESCROW itasoma tarehe 26/11/2014 but sijui muda naomba kujuzwa. Asanteni
 
Sipati picha ila ninavyoijua hii nchi nadhani habari tutaisoma magazetini. Tena nadhani hata wa kutolewa kafara wameshaandaliwa.
 
wadau
naomba kufahamishwa leo ndio siku ya kusomwa report ya cag bungeni au nikesho?naomben majibu wadau wengine wanasema leo wengine kesho
 
wadau
naomba kufahamishwa leo ndio siku ya kusomwa report ya cag bungeni au nikesho?naomben majibu wadau wengine wanasema leo wengine kesho

tarehe 26 Jumatano, ungesoma thread za wengine ungejua badala ya kuanzisha mpya
 
Back
Top Bottom