Naomba kujuzwa kuhusu sifa za kufanya mtihani wa kidato cha 6 kama school candidate

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Mungu ni mwema mdogo wangu amefaulu kwa kupata daraja la kwanza na alama 16 (1 point 6). Physics na Mathematics amepata D. Ila Biology B, Chemistry B na Geography C. Lengo lake lilikuwa ni kusoma PCB, PCM au EGM. Hataki CBG.

Kwenye PCB au PCM tayari Physics ana D. Kwenye EGM tayari Math ana D. Je, inawezekana akaruhusiwa kusoma PCM, PCB au EGM. Maana mimi najua ufaulu unaoruhusiwa ni alama C. Naomba mwongozo wakuu wale mliobobea katika nyanja hii nyeti ya Elimu.

Natanguliza shukrani zangu.​
 
Si anabadilisha shule huko huko au siku hizi mambo yamekua magumu?
 
PCB anapiga vizuri tena government. Mimi mwaka jana dogo alipata Physics D Chemistry B math B now anapiga PCM government
 
Back
Top Bottom