Naomba kujuzwa kuhusu Mbegu hizi ambazo nimepewa huko Moshi - Kilimanjaro

Jambo Tz

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
670
202
Haloo wadau nimekwenda Moshi nikakutana na hizi mbegu wasema ni kama karanga na zinatibu maradhi wenye ujuzi nazo tafadhali
IMG_8888.jpg

IMG_8889.jpg


Tujuzane natanguliza zangu shukrani
 
Hizo unatafuna tu, tamu kama karanga,, ukitaka unakamua unakunywa juice,, ni kama maembe tu,,
 
Hizo zinaitwa kweme. Unaweza choma kwenye moto au ukapasua ukatoa kilichopo ndani ukatwanga ukaeka kwenye mboga au ndizi
 
Mbegu😁😁😁

Ni kweme hizo siyo sperm.

Ni jamii ya karanga.

Mti wake hutambaa juu ya mti mkubwa Kama ufanyavyo mpassion. Huzaa natunda makubwa ambayo ndani yake vipo hivyo vimbegu kweme.

Kweme ndogo ni jike na ndiyo huzaa. Kweme kubwa ni madume. Dume hutambaa na kutoa maua tu ila halizai.

Tunda/ bunda la kweme likikomaa huoza/kuiva na kudondoka ambapo kweme husambaa chini ya mti.

Niwewahi kuotesha na kuvuna.

Bunda la kweme lina kishindo kukubwa sana likidondoka
 
Nimezikula sana maeneo ya Mbeya Tukuyu miaka hiyo.....kuhusu kutibu maradhi sijui itakua inatibu maradhi gani.........nataman iwe ni matatizo ya moyo au nguvu za kiume.
 
Shukran ndugu je za kuchoma amaaa kukaanga
unabandua hilo ganda lake kisha unakangaa kama karanga(huweki mafuta) tjen unazisaga zinakuwa kama karanga za kusaga vile, unapikia kwenye mboga, uji(inafanya kazi kama nazi vile)
 
Aiseee.. i miss Rombo. Nimemiss kweme jamani
Unazichoma hizo. Tunawekaga kwenye majivu ikiica unapasua unakula
 
Back
Top Bottom