Naomba kujuzwa kuhusu maisha ya Same mjini

Mkuu umenikumbusha nyumbani wakati mpango wa kwenda huko ni desemba, mi niwaishinde nusu jangwa pale ila napapenda kwetu acha mzaha.
Ishinde unafahamu ile familia ya marehemu mzee Onesmo Mziray ambaye ana mwanae Padri mziray, Adella na wengineo?
 
Same ni miongoni mwa miji inayokuwa Kwa kasi. Mji unamahitaji yote muhimu ikiwa ni pamoja na huduma za afya, barabara nzuri, huduma za kibenki, Elimu na umeme.

Same unaweza kusafiri muda wowote kwenda mikoa kama Arusha, Dsm na morogoro kutokana na uwepo wa Highway itokayo Nairobi-Arusha-Moshi- mpaka Dsm, Moro, Dom, na mbeya.

Changamoto.
1. Uhaba wa maji
2. Ukame na jua Kali nyakati za mchana wakati usiku baridi kali.
3. Vumbi.

Burudani.
Same kuna Bar kadhaa ambazo mtu huweza kwenda kuburudika na kustarehe huko.
Japo kuna kiwango kidogo cha Madadapoa.

Hakuna vigodoro wala singeli.

Warembo wengi wa same ni wafupi na wachache wakiwa warefu wa wastani japo warefu wapo Kwa nadra sana. Rangi zao wengi ni Maji ya kunde na weupe japo weusi wapo kidogo.

Tabia za wanawake wa Kipare hasa Same.
1. Wengi wanajisikia na kujiona yaani ni masikini jeuri.
2. Wanamsimamo wa Kati hasa kwenye ishu za kutongozwa. Yaani sio rahisi kukubali wala si rahisi kukataa.

3. Hawana tabia za kusutana.
4. Hawana tabia za kukushobokea.

Mila na desturi.
1. Mara nyingi ukiwa Same utasikia watu wakiongea Kipare. Hivyo hii inaweza kuwa changamoto.

2. Uchawi upo kiasi japo huko milimani ndio kitovu.

3. Chakula chao kikubwa ni Makande, kibulu, kishumba n.k.
Makande hupikwa zaidi Ijumaaa kwani wengi ni Wasabato.

4. Pombe ya kienyeji ni Denge
5. Kuna janja lakini siku hizi mara moja moja. Janja ni dansi ya Kipare ambayo huchezwa nyakati hasa za jioni

Fursa za Kiuchumi
1. Biashara ya maji ni nzuri kwani hiyo ndiyo changamoto ya mji huo.

2. Nguo sio sana.
3. Biashara ya mazao na matunda. Kutokana na mji kukumbwa na ukame wa mara Kwa mara.

Karibu same mkuu, huko ndiko niliposomea na kukulia.
 
Ule mradi niliacha umefika pale Mgagau-Mnadani,hivi unategemewa kumalizika lini?Shida ya huo mji ni maji,tabu sana ya maji hapo...Yanapatikana ya chumvi ambayo yanaharibu sana nguo.

Nilikaa Same miezi minne kikazi.Nilifikia sehemu moja inaitwa Elephant Motel.Ipo pembeni ya mji.Chakula hasa matunda na mengineyo,yanapatikana kwenye gulio la Kwasakwasa,gulio lipo kila J'pili,watu wanashuka na vyakula toka milimani,hapo maji ndio tatizo.

Jumamosi maduka mengi yanafungwa sbb wenyeji wengi ni Wasabato.Ila watoto wa Kipare ukimuonja tu,lazima akupandie milimani akutulize.Bar kubwa ni PADEKO na Kimweri karibu na kituo cha Mafuta cha Panone.

Wilaya ina ukame sana,jua kali sana lakini usiku kuna baridi ya upepo(kipupwe),na vumbi kubwa sana ndio maana wadada wengi wanavaa open shoes na soksi.Nyumba za kupanga si gharama sana.

Wewe mkuu unaenda kuwa mtumishi wa Serikali au shirika binafsi?
 
Asante sana kwa maelezo...ni shirika binafsi
 
Kwanza kabla ya yote nakukaribisha sana kwetu. Same ni eneo ambalo kuna wakati kunakuwa na ukame wa hali juu. Sisi wenyeji wa Same (wapare) ni wakarimu, hatuna majungu, upande wa dini wengi wengi ni sabato. Karibu sana sana wenyeji tupo tutakupokea karibu mpendwa wetu wilayani Same

Dah, mkuu umenikumbusha mbali sana, miaka kadhaa nyuma wakati nasoma hapo Same sec kuna mdada mmoja hivi msabato moyo ulimdondokea hadi nikajikuta na mimi nimekuwa msabato kwa kwenda kanisani kwao ili tu nipate kumuona maana alikuwa geti kwao ni shida.

Same, nimepamiss sana pamoja na ukame na upepo wake ukianza kuvuma kama tuko Sahara.
 
Hili ulitarajie pia kuwa ukihamia na kuishi hapo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja aidha uwe unapenda kujichangamya na watu au hupendi watakuwa wamekufahamu watu wengi sana yaani ni mashushushu kinoma. Na hii imewasaidia sana kiusalama ndio maana hakina jambazi anaweza kuja na kujifi ha Same. Kwa maneno mengine wanapenda sana kujua maisha ya watu hasa wageni.
 
Kuna miti wajerumani waliotesha kule milimani ina kunywa maji balaa, na kuna jiwe la nyoka naskia wajapani waliliiba wakati wana tengeneza barabara ya hedarh
 
Kwanza kabla ya yote nakukaribisha sana kwetu. Same ni eneo ambalo kuna wakati kunakuwa na ukame wa hali juu. Sisi wenyeji wa Same (wapare) ni wakarimu, hatuna majungu, upande wa dini wengi wengi ni sabato. Karibu sana sana wenyeji tupo tutakupokea karibu mpendwa wetu wilayani Same
kumbe wewe n mtani wangu? chedi avae
duh ila ukame wa same n hatari
 
1495608692756.jpg
1495608709870.jpg
1495608722558.jpg
1495608730699.jpg
1495608741042.jpg
1495608754214.jpg
 
Back
Top Bottom