Naomba kujuzwa kuhusu maisha ya Same mjini

gudJohnson

Member
Aug 24, 2015
34
56
Habari za Leo wanajukwaa, kama heading inavyosema, natamani kupata highlights za maisha katika mji wa Same mkoani Kilimanjaro. Nimepata uhamisho kwenda Same, so naomba kujuzwa hali ya maisha hapo Same, fursa zilizopo na information yoyote kuhusu Same unayoona ni muhimu. Ahsanteni sana
 
Hili ndilo eneo la kituo chako kipya cha kazi...
upload_2017-5-23_8-18-54.png
 
Kwanza kabla ya yote nakukaribisha sana kwetu. Same ni eneo ambalo kuna wakati kunakuwa na ukame wa hali juu. Sisi wenyeji wa Same (wapare) ni wakarimu, hatuna majungu, upande wa dini wengi wengi ni sabato. Karibu sana sana wenyeji tupo tutakupokea karibu mpendwa wetu wilayani Same
 
Same pazuri sana mradi mkubwa wa maji umefika hakutakuwa na shida ya maji kama awali. Utafanya mengi nenda ujionee ila fanya kilichokupeleka achana na vidosho utapata shida kubwa sana..
Ule mradi niliacha umefika pale Mgagau-Mnadani,hivi unategemewa kumalizika lini?Shida ya huo mji ni maji,tabu sana ya maji hapo...Yanapatikana ya chumvi ambayo yanaharibu sana nguo.

Nilikaa Same miezi minne kikazi.Nilifikia sehemu moja inaitwa Elephant Motel.Ipo pembeni ya mji.Chakula hasa matunda na mengineyo,yanapatikana kwenye gulio la Kwasakwasa,gulio lipo kila J'pili,watu wanashuka na vyakula toka milimani,hapo maji ndio tatizo.

Jumamosi maduka mengi yanafungwa sbb wenyeji wengi ni Wasabato.Ila watoto wa Kipare ukimuonja tu,lazima akupandie milimani akutulize.Bar kubwa ni PADEKO na Kimweri karibu na kituo cha Mafuta cha Panone.

Wilaya ina ukame sana,jua kali sana lakini usiku kuna baridi ya upepo(kipupwe),na vumbi kubwa sana ndio maana wadada wengi wanavaa open shoes na soksi.Nyumba za kupanga si gharama sana.

Wewe mkuu unaenda kuwa mtumishi wa Serikali au shirika binafsi?
 
Fuata kilichokupeleka, waheshimu wenyeji nao watakuheshimu ukilete mikwara watakunyoosha. Ningekupa mifano lakini itaathiri wahusika maana bado wapo.
Kama ni mtu wa kuelewa ameelewa kwa kweli hata sisi kule kwetu ukienda kichwa kichwa ukaanza kuvamia vya watu utatolewa busha
 
View attachment 513085
Nimeikumbuka elephant hotel aiseeee......
View attachment 513086
View attachment 513087
Duhhh.......
Sikuzile nili furahia maisha walau kwa siku saba, nikiwa vacation pale same....
Same kuna watoto wazuri kama roho yangu aiseeeee....
Umenikumbusha mbali sana.Nimelala hapo miezi minne na nusu,nilikuwa hapo kikazo mwaka 2015.
Hapo kushoto ya kuingia reception kuna miti mingiii na mahali pa michezo ya watoto na kupumzikia.

Niliipenda ile mandhari sbb ya hali ya hewa ya Same,ukiwa Elephant Motel hata mchana unakaa nje chini ya miti.Kweli miti ni hazina,tupande miti kuukabili ukame.
 
Nimefika mpaka kalimawe unaweza lima nyanya na matikiti kuna mito mingi tu ila hawana maji ndani
 
Back
Top Bottom