Japo siifahamu hiyo kampuni، lakini nina fahamu baadhi ya kampuni ambazo zinajihusisha na uuzaji wa virutubisho kama Forever, BF SUMA, Neo Life nk
Kwa maoni yangu hizo ni biashara kama biashara nyingine, na sio utapeli.
ila ni ngumu mno kufanikiwa kwenye biashara hizi, kimsingi zinahitaji nguvu kubwa kuliko hata biashara za mtaani.
1. Gharama za kuanzia ni kubwa
2. Gharama za kuendeshea ni nyingi; kuhuhuria semina , bando la kutosha, kulipia matangazo, kuwalipa mentors wakufunze biashara.
3. Gharama za bidhaa ni kubwa mno kiasi kwamba watu wengi hawawezi kununua, mfano kipindi hicho nafanya dawa ya mswaki ilikuwa 23,000 ambapo kwa Sasa nadhani itakuwa ni zaidi ya 25,000
4. Sio biashara za kutegemea mafanikio ya haraka kama inavyosemwa, yaani unatakiwa ujipe muda angalau zaidi ya mwaka wa kujijenga tu bila kupata faida
5. Hizi biashara unaweza kukaa Hadi miezi 6 hujapata mteja hata mmoja.
6. Kuna mentor wangu mmoja aliwahi kuniambia; usinione na mafanikio haya na namna navyoeleza mafanikio kwa urahisi ila nimepitia shida miaka miwili biashara ilikuwa haifanyiki ila siwezi kusema kwenye semina.
7. Kama huwezi kuongea; mdomo mzito kama umemeza keki ya 500, kama mbali na hizi kazi
NB
Kwa mtu anayejitafuta usijaribu kuingia kwenye hizi biashara huku ukitegemea mafanikio ya haraka
Ni kweli baadhi ya watu wachache wanafanikiwa (nathibitisha Hilo) ila wengi zaidi (asilimia zaidi ya 80) wanafeli
AKILI KICHWANI