Naomba kujuzwa kuhusu Biashara ya uwakala wa bima

Jf kwa kipindi chote imekuwa na wataalamu mbalimbali.

Naomba kujua maokoto au makadilio ya maokoto ya wakala wa bima(gari) katika bima moja yapo vipi.

Natanguliza Shukurani...
Ukiwa umesajiliwa kama wakala, utalipwa 12.5% ya kila kiwango (ukiondoa VAT) utakachopeleka kwenye kampuni ya bima.

Mfano third party premium ya gari dogo ni 118,000/-. Ukitoa VAT inabaki 100,000/-. So utalipwa 12,500/- kama commission.
 
Sinayo uzoefu sana na hiyo biashara, ila kwa kipindi kidogo nilichofanya ni biashara nzuri na Comission yake si haba Maana unachukua 12.5/% Ya premium aliyolipa mteja baada ya kutoa VAT. Mfano rahis ni kuwa Third Paty (Bima ndogo) ya Gari binafsi Mteja analipia 118,000/= Kati ya hiyo 100,000/= ni net Premium ambayo ndio Comission yako inatoka sawa na Tsh. 12,500/=

So Comission inalipwa kwa mfumo huo kwa kila gari utakayo ikatia Bima. Ila ieleweke pia kuna Bima kubwa (Comprehensive) na Bima Ndogo (Third Party) Bima kubwa zina Comission nzuri zaidi maana mteja analipa zaidi hivyo ukiwa na mtaji wa wateja watakao kuwa wanakata Bima kubwa basi unanafasi ya kutengeneza kipato kikubwa zaidi. Pia kuna hizi gari za Biashara kwa maama Hiace, Mabasi na Gari za Mizigo. Hizi gharama zake za Bima zinachajiwa kulingana na Idadi ya siti kwa gari za abiria na Ton kwa gari za Mizigo. Pia hizi zina Comission nzuri Kikubwa ni kupambana kutafuta wateja

Kuna kitu nimeona siku hizi ambacho kwa kias flani ni changamoto kwa Mawakala wa Bima. Tangu kuingia kwa Mabenki na Makampuni ya Simu kwenye huduma hii ya Bima kama ma Broker au Insurers wao wamekuwa na njia tofauti tofaut za kupata wateja, Mfano Mitandao ya Sim yenyewe inawakopesha wateja kwa maana ya kuwa wanakatiwa Bima ya mwaka mzima ila wao watalipa Premium polepole kwa kipindi watakacho kuwa wamekubaliana, Kwa Mabenki ni kuna uvumi kuwa Wateja wanapoenda kuomba mikopo kwao wamakuwa wakipewa kipengere cha kuwataka Gari wanazomiliki wakatie Bima Kwao lakin pia nao nasikia k wanawakopesha wateja wao Bima. Ni kwa nini Mkopo wa Bima ni changamoto kwa mawakala, ni kwa sababu Mfumo wa Bima hauruhus mkopo wa Bima, Unamtaka mteja kulipa kias chote ili apatiwe Bima, hivyo basi kama huna mtaji wa Cashi kwa maana Kumkopesha mteja wako basi anaweza kukukimbia.

Vigezo vya kuwa wakala wa Bima, Cha kwanza kabisa lazima uwe umesoma kozi ya Bima japo kwa Level ya Chini kabisaa yaani COP, Gharama za usajili ni za kawaida kabisa na mtu yeyote anaweza kumudu
 
Mtaalam nimekupata vyema.
 
Back
Top Bottom