Naomba kujuzwa haya kuhusu Homa ya Ini, Homa ya Manjano

real hustler

New Member
Mar 12, 2021
4
2
Habari za majukumu,

Niko hapa nikiwa na kuchanganywa na vitu vifuatazo. Ambavyo ningeomba msaada

1. Kuna tofauti gani Kati ya chanjo ya homa ya Ini na yellow fiver

2. Sina maambukizi pia sijawahi chanjwa nimepata mwaliko wa safari za kimataifa, nauliza ni hospitali zipi naweza pata huduma hiyo na Kati ya hizo ni ipi muhimu/ inayohitajika kwa msafiri wa kimataifa

3. Ni lazima uwe na kadi ya chanjo hiyo airport

4. Gharama za chanjo

5. Kama unafahamu hospital inayotoa huduma hiyo ni masaa gani wanatoa huduma hiyo. Au ni siku gani hutoa huduma hiyo

Binafsi napatikana Morogoro, hiyo ni Safar yangu ya kwanza kupanda ndege

Karibuni na asanteni kwa msaada wa kimawazo
 
Homa ya ini ni kwa kimombo ni (hepatitis) na inasababishwa na vitu mbali mbali ila kwa ambayo ni ya umuhimu zaidi kiafya ni Hepatitis B inayosababishwa na kirusi cha hepatitis B na inayosambazwa kwa kugusana na maji maji ya mwili.
Yellow fever ni Homa pia lakini inasambazwa na mbu aina ya aedes.
Zote Zina chanjo na ni za muhimu kwa wanaosafiri kwenda maeneo yanayotambulika kuwa na changamoto hizo.
Hepatitis huwa inachomwa kwa series kama tatu (sifahamu kuhusu yellow fever). Ila pia unaweza ukapata kimchongo japo ni hatari kwa afya yako incase ukaukwaa ugonjwa ndipo utaona changamoto yake.
Yellow fever andaa kama 50,000_70,000 na hepatitis 30,000-100,000 kwa makadirio ya haraka haraka.
NB:Zote mbili ni muhimu kwa airport, ila sio kwa sababu ya safari tu ila at least uwe na hepatitis B kwa kujilinda mwenyewe.
Wengine wataendelea na kuongeza/kukosoa nilipokosea.
 
Habari za majukumu,

Niko hapa nikiwa na kuchanganywa na vitu vifuatazo. Ambavyo ningeomba msaada

1. Kuna tofauti gani Kati ya chanjo ya homa ya Ini na yellow fiver

2. Sina maambukizi pia sijawahi chanjwa nimepata mwaliko wa safari za kimataifa, nauliza ni hospitali zipi naweza pata huduma hiyo na Kati ya hizo ni ipi muhimu/ inayohitajika kwa msafiri wa kimataifa

3. Ni lazima uwe na kadi ya chanjo hiyo airport

4. Gharama za chanjo

5. Kama unafahamu hospital inayotoa huduma hiyo ni masaa gani wanatoa huduma hiyo. Au ni siku gani hutoa huduma hiyo

Binafsi napatikana Morogoro, hiyo ni Safar yangu ya kwanza kupanda ndege

Karibuni na asanteni kwa msaada wa kimawazo
1. Kuna tofauti kati ya chanjo ya Hepatitis na yellow fever

A: Hepatitis: ni kitendo cha ini kututumka kutokana na kuathiriwa na matatizo (matumizi makubwa ya pombe, madawa makali, utunzaji mkubwa wa mafuta/fatty liver) NA ikiwemo virusi kama Hepatitis B na C.

Hivyo, chanjo huwa ni dhidi ya virusi husika na lengo ni kudhibiti ugonjwa dhidi ya kurusi cha Hepatitis B . Ingawa kwa sasa kurusi C hakina chanjo.

B: Yellow fever: ni ugonjwa unaotokana na maambukizi ya virusi aina ya Flavivirus ambavyo huenezwa na mbu.

Hivyo, chanjo huwa ni dhidi ya virusi husika na hatimaye ugonjwa wa Yellow fever.

2. Kwa Dar es salaam, hospitali ya Mnazi mmoja iko na muunganiko mzuri, wa bei nafuu na unaoaminiwa wa chanzo mbalimbali hitajika. Pia kuna hospitali kama Aga Khan kubwa.

Chanjo gani muhimu hutegemea pia nchi unayokwenda. Ni muhimu kuwasiliana na Ubalozi au kujifunza haya kupitia mtandao wa Ubalozi husika, unaweza kupata maelezo zaidi.

3. Ni lazima uwe na kadi ya chanjo hiyo airport. Jibu ni ndiyo, kwani kufika nchi husika bila kutimiza masharti inaweza kuwa chanzo cha usumbufu mkubwa kwako.

4. Gharama za chanjo:
Wasiliana na hospitali husika kwa kupata namba zao hata kwenye mtandao ili kupata maelezo halisia.

5. Siku na saa: mawasiliano yako na wao yatamaliza hili.

MNAZI MMOJA HOSPITALI
SIMU: +25524 223 1614

AGA KHAN HOSPITALI
SIMU: +25522 234 4100
 
Back
Top Bottom