Naomba kujuzwa gharama za tiles hizi

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
5,685
6,489
Habarini wakuu.

Niende moja kwa moja kwenye topic. Wakuu nina nyumba yangu ipo hatua ya finishing ina square meter 206. Nyumba iko Moshi.

Kwa vile sipo karibu nikamuomba fundi anipe makadirio ya tiles na akaniletea makadirio kama ifuatavyo

50×50 box 118
40x40 box 11
25×40 box 82
Skating box 11

Nataka niweke tiles ambazo ni za bei ya kawaida ambazo zinadumu. Naombeni ushauri niweke zipi? Na naombeni bei ya box tajwa hapo juu nijiandae maana hadi kichwa inapata moto kila nikiwaza bado aluminium, skimming na mauchafu mengine.

Pia naomba kujua kama kuna uwezekano nikapata sehemu nikawa nalipa kidogo kidogo maana hela haikai.

Natanguliza shukrani
 
Habarini wakuu. Niende moja kwa moja kwenye topic. Wakuu nina nyumba yangu ipo hatua ya finishing ina square meter 206. Kwa vile sipo karibu nikamuomba fundi anipe makadirio ya tiles na akaniletea makadirio kama ifuatavyo

50×50 box 118
40x40 box 11
25×40 box 82
Skating box 11

Nataka niweke tiles ambazo ni za bei ya kawaida ambazo zinadumu. Naombeni ushauri niweke zipi? Na naombeni bei ya box tajwa hapo juu nijiandae maana hadi kichwa inapata moto kila nikiwaza bado aluminium, skimming na mauchafu mengine.

Pia naomba kujua kama kuna uwezekano nikapata sehemu nikawa nalipa kidogo kidogo maana hela haikai

Natanguliza shukrani
Hongera na pole kwa huu mziki mnene unaokusubiri.. Sina hakika na hiyo idadi pengine nyumba ni kubwa mimi nakupa tu makadirio
50 kwa 50 ni kati ya 40,000 mpaka 60,000
40 kwa 40 ni kati ya 35,000 mpaka 45,000
25 kwa 40 ni kati ya 30,000 mpaka 40,000
Skating ni kati ya 32, 000 mpaka 37,0000

Ushauri wangu
1.Anza na sehemu nyeti kama sebuleni vyooni, na koridoni nk

2. Kuna baadhi ya maeneo weka zile zinazoitwa grade B kwa maana ya kwamba zimemeguka kidogo kwenye pembe ama rangi haikakolea kivile nk
Wengi huokoa gharama mpaka 40% kwa kutumia hizo na huwezi kujua kwakuwa kama unaweka 50 kwa 50 unanunua 60 kwa 60 kisha fundi anazi size kuwa 50 kwa 50 na kuondoa mapengo yote
Kuna uhuni mkubwa kwenye hii biashara kwakuwa baadhi ya wauzaji huchukua grade B na kuzi size na kuuza bei ya punguzo ambalo sio kubwa.. Na mafundi nao hufanya hivyo ukiwapa hela

3. Pata mtu wa kiwandani ama wa sales ambaye ana wateja wa jumla ili akuchomeke kwa wateja wake upate kwa bei ya jumla

Ukihitaji msaada zaidi nicheki.. Nina madirisha na milango ya PVC used ya ulaya very high quality na ni double glass kwa bei ya kutupa
Milango ya ndani pia ninayo
 
Hizi hapa ni 50 kwa 50 bei ni Tsh 32,000 kwa box
IMG-20220326-WA0045.jpg
IMG-20220326-WA0044.jpg
IMG-20220326-WA0043.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom