Naomba kujuzwa zinapouzwa CD za majibu ya X-ray mahospitalini

Whitney Houston

JF-Expert Member
Jan 5, 2019
213
403
Wakuu poleni na majukumu,

Naomba kwa anaefahamu anijuze zile CD ambazo huwekwa majibu ya X-ray ya mgonjwa zinauzwa wapi kwa MWANZA?

Mgonjwa alipigwa X-ray siku ya ijumaa wiki iliyopita ktk hospital ya serikali hapa Mwanza na ikagundulika mshipa wa kwenye nyonga umekatika,sasa tuliandikiwa rufaa tumpeleke Bugando kwajili ya Tiba zaidi ILA dokta akasema turudi kitengo cha X-ray kuchukua CD yenye majibu tuende nayo huko Bugando.

Hapo kitengoni tukakuta CD zimeisha kwahyo tukapewa kipande cha box la hiyo CD tukaitafute madukani ikiwa empty ipelekwe hapo hospital tuwekewe majibu. Sijafanikiwa kuipata hiyo CD mpaka sasa kwakweli.

Tokea hyo Ijumaa mgonjwa yupo tu nyumbani na hatembei wala ku move kutokana na hitilafu ktkt nyonga na CD ya kwenda nayo Bugando imekua ni vigumu kukupata.

Naombeni kwa anayejua zinauzwa ktk maduka ya aina gani anijulishe.

Shukran.

IMG_20230918_211354.jpg
 
Back
Top Bottom