Naomba kujuzwa bei ya Phantom X

mtume wawatu

JF-Expert Member
Oct 30, 2016
748
1,000
avechi 4GB/64GB version ni 324,000, 128gb version ni 361,000. kama una mtu unamjua itaongezeka kama 20,000 mpaka kukufikia. Avechi wenyewe kukutumia wanachrage 2500 (53,000).

hivyo kivyovyote haifiki laki 4, Tigo wanauza laki 5.
Ndo maana hawatangazi we
 
vidmate

JF-Expert Member
May 7, 2018
533
1,000
Kitu kinaweza kuwa bora zaidi lakini kisiwe bora kwenye battery. Kwenye mambo ya tech huwa Kuna fomula moja
-compact
-good battery life
-perfomance

Chagua viwili kati ya hivyo, huwezi kamwe kupata vyote vitatu.

S na note ndio best kwenye samsung hizi zina kila kitu kuanzia processor zenye nguvu, vioo vizuri, na zipo pia zinazokaa na chaji kiasi ila si sana kama A Na M. Bei zake ni ghali.

J series hizi ni zilipendwa siku nyingi wameacha kuzitoa.

A series zenyewe hazina display na processor kali Kama S na note ila zina mabattery makubwa kushinda S, bei zake ni za kati na ndogo. Na mara nyingi hupatikana Dunia nzima.

M ni kama A Sema zipatikana masoko maalum kama India na baadhi ya Nchi zenye wateja wengi.

Kuhusu suala Zima la ubora ni note na S series.

Kuhusu ukaaji chaji ni M series zinakaa na Chaji sana, Sema ni mpaka uagizishie nje kwa hapa Tz.

Kama hutaki kuagizishia nje hata A zinakaa na Chaji kiasi chake.

Mwisho wa siku ni wewe na Budget yako, zipo A, M, s Na note za bei mbalimbali.
Mkuu naomba uizungumzie kdg Red mi note 10 pro max
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
26,222
2,000
Mkuu naomba uizungumzie kdg Red mi note 10 pro max
Note 10 pro max ni version ya India, huku kwetu inajulikana kama Note 10 pro tu bila neno max.

Na lisikutishe hilo neno Max, inafanana kila kitu na note 10 pro, kasoro tu haina NFC na ip rating.

Hivyo vyema kununua Note 10 pro ambayo ni bei rahisi zaidi, na ina vitu vingi kushinda note 10 pro max.

Kuhusu ubora wake ni simu nzuri all around kwa watu wenye matumizi ya kawaida.
 
vidmate

JF-Expert Member
May 7, 2018
533
1,000
Note 10 pro max ni version ya India, huku kwetu inajulikana kama Note 10 pro tu bila neno max.

Na lisikutishe hilo neno Max, inafanana kila kitu na note 10 pro, kasoro tu haina NFC na ip rating.

Hivyo vyema kununua Note 10 pro ambayo ni bei rahisi zaidi, na ina vitu vingi kushinda note 10 pro max.

Kuhusu ubora wake ni simu nzuri all around kwa watu wenye matumizi ya kawaida.
Mkuu kwani red mi note 10 na note 10 pro zina tofauti sana?

Vipi bei zake hapa bongo zikoje kwa upande wa note 10, note 10 pro na hiyo note 10 pro max
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
26,222
2,000
Mkuu kwani red mi note 10 na note 10 pro zina tofauti sana?

Vipi bei zake hapa bongo zikoje kwa upande wa note 10, note 10 pro na hiyo note 10 pro max
Kama nilivyokwambia juu pro max ni ya India tu, haipo kwengine.

Na ndio kuna utofauti mkubwa baina ya 10 na 10 pro.

Kwa Tz hazipo official hivyo bei ni ghali ila kwa kenya note 10 ni inakaribia laki 4 na 10 pro Ina karibia laki 6
 
vidmate

JF-Expert Member
May 7, 2018
533
1,000
Kama nilivyokwambia juu pro max ni ya India tu, haipo kwengine.

Na ndio kuna utofauti mkubwa baina ya 10 na 10 pro.

Kwa Tz hazipo official hivyo bei ni ghali ila kwa kenya note 10 ni inakaribia laki 4 na 10 pro Ina karibia laki 6
Shukran kk meagiza India pro max laki 7 hapo ni nje ya gharama za usafiri na hiyo note 10 ilikuwa around 450
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom