Naomba kujua sheria ya utata huu

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,095
4,059
Kuna matukio mawili yameacha UTATA na kupelekea kuvurugika kwa mechi mbili tofauti.

1. Golikipa alishika mpira na baada ya kushika vizuri, fowadi alikuwa mitaa ile ndani ya 18. Kwa mshangao golikipa alimpiga Pepsi bila sababu, refa alifunika tuta. Jambo ambalo lilipelekea mchezo kuisha. Baadhi wanasema ni faulo na wengi walidai ni penalty dhahiri.

NAOMBA ufafanuzi.

2. Kuna timu ilifika uwanjani bila golikipa na iliwabidi mchezaji mmoja akae golini. Baada ya dakika Kama 30 golikipa alifika na timu ikafanya sabu ya mchezaji mwingine na kuingia golikipa ili sasa golikipa asilia aende golini na aliyekuwa golini aingie ndani. Mzozo ulitokea kwa kigezo kuwa aliyekuwa golini hatakiwi kucheza ndani badala yake atoke nje. Je, sabu ya aina hii ipo?
 
La kwanza kipa alifanya faulu baada ya kudaka, hapo kipa alitakiwa apewe kadi, lingekuwa tuta iwapo kipa angefanya faulu wakati anaokoa mpira.

Kuhusu la pili hakuna tatizo ili mradi kabla ya kuanza mpira kila timu ilikuwa na wachezaji 11.
 
Uyo golikipa wa muda anaruhusiwa kuingia kucheza ndani baada ya kufanya sub ya mchezaji mmoja ili kupisha kipa og akae golini.
 
Back
Top Bottom